Taarifa ya kuitwa kwenye usaili - TBS

Shirika la Viwango Tanzania linapenda kuwatangazia waombaji wote wa nafasi za Senior Marketing Officer II, Quality Assurance Officer II, Standards Officer II, Metrologist II, Laboratory Technician II, Laboratory Assistant II, Maintenance Engineer II, Human Resource Officer II, Driver II, Personal Secretary II, Assistant Accountant II, Accounts Technician II, Records Management Assistant I, Records Management Assistant II, Librarian II, Assistant Internal Auditor II, Computer System Technician I, Legal Officer II, Editor II, Corporate and Public Affairs Officer II, Maintenance Technician II, kuwa kutakuwa na mtihani wa kuandika kuanzia tarehe 31.07.2014 mpaka tarehe 01.08.2014 katika ukumbi wa Yombo (University of Dar Es Salaam).

Wasailiwa wanashauriwa kuzingatia yafuatayo:

1. Kuja na vyeti halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne na vyeti vya Taaluma ambayo mtahiniwa aliomba.

2. Mtahiniwa atakaye shindwa kuja na vyeti Halisi atakuwa amejiondoa katika usaili.

3. “Transcript”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo ya kidato cha nne na
sita HAVITAKUBALIWA.

4. Kila msailiwa aje na kitambulisho kinachomtambulisha.

5. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.

6. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanya usaili.

7. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa.

Limetolewa na:

Kaimu Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania,
S.L.P. 9524,
DAR-ES-SALAAM

Tafadhali bofya linki ifuatayo kupata orodha ya walitwa kwenye usaili: