Na Winner Abraham -- Serikali yatiliana saini ya makubaliano ya msaada wa kimaendeleo na Jamhuri ya watu waKorea ambapo katika makubaliano hayo jumla ya Dola za Kimarekani zaidi ya 100 kwa ajili ya mikopo nafuu na dola milioni 10 kama msaada kutoka shirika la Mendeleo la Kimataifa la Korea (KOICA)
Makubaliano hayo yametiliwa saini baina ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile na Balozi wa Serikali ya Korea hapa nchini Chung IL.
Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile amesema kuw a makubaliano hayo yatasaidi katika
kutekela baadhi ya miradi ya MKUKUTA hasa katika sekta zilizoanishwa katika mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) zikiwemo sekta za Kilimo, Maji, Nishati na Afya.
Dkt. Likwelile ameongeza kuwa kupitia makubaliano hayo Serikali inatarajia kupata wataalam wa sekta mbalimbali watakao kuja nchini kwa ajili ya kujitolea katika Taasisi mbalimbali hapa nchini, hivyo nimatarajio yake kuwa itaongeza ufanisi katika utekelezaji wa makubaliano hayo.
“Ni matumaini yangu kwamba kupituia makubaliano haya nchibni yetu itanufaika kwa kiasi kikubwa sana ukizingatia kwamba richa ya msaada wa kifedha tutakoa pata lakini pia kundi la Wataalamu takribani 100 kutoka Korea wanatarajiwa kuja nchibni kufanya kazi za kujitolea katika sekta za Afya, Kilimo, Elmu na sekta nyingine.”
Alisema Dkt. Likwelile.
Aidha Dkt. Likwelile ameishukuru Serikali ya Korea kwa msaada huo na kuahidi kuwa utekelezaji wa miradi mbalimbali itakayokuwa china ya makubaliano hayo itafanya kwa ufanisi wa hali ya juu ili kujengea heshima baina ya nchi hizi mbili.
Kwa upande wake Balozi wa Serikali ya Korea nchini Tanzania Chung IL ameeleza kuwa Tanzania imekuwa ni nchi maja wapo katika Bara la Afrika zinazopata misaada kutoka Korea hivyo ni matumaini yake kwamba itapiga hatua na hatimaye kukuza uchumi wake.
Balozi Chung IL amesema kuwa makubaliano waliotiliana saini leo yatasaidi Tanzania kupiga hatua katika sekta za Afya, Kilimo, Maji na Nishati ambazo ni huduma muhimu kwa jamii yake.
Hii siyo mara ya kwanza kwa Serikali ya Jamhuri ya Korea kutoka misaada kwa Tanzania,ambapo mpaka sasa baadhi ya miradi iliyogharimu kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 22.7 imekamilika ambayo ilihusisha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Chuo cha Dar es Saalam Sehemu ya Uandisi,uboreshaji wa Vituo vya Afya na miradi kadhaa iliyotekelezwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.