UDASA: Kongamano la kujadili mchakato wa kupata Katiba Mpya

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) imeandaa kongamano la kujadili mchakato wa kupata Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kongamano hilo litafanyika tarehe 27 Julai 2014 siku ya Jumapili kuanzia saa 8 mchana ndani ya ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kongamano hilo litarushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Star TV.

Mada kuu ya kongamano hilo ni, “Tujadili na Kutafakari Mchakato wa Katiba Mpya kwa
Manufaa ya Taifa Letu”.

Watoa Mada katika kongamano hilo ni Prof. Y. Msanjila na Dkt. Kitila Mkumbo.

Tunapenda kuchukua fursa hii kwa heshima kubwa kuwakaribisha wananchi wote ili wawe miongoni mwa watu watakaotoa mchango wao mkubwa katika mchakato wa kuleta maridhiano ya kitaifa kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya ya taifa letu la Tanzania.

Tutanguliza shukrani zetu za dhati kwa ushiriki wako kwenye kongamano hili.

Imetolewa na
Faraja Kristomus.
(Katibu – UDASA)
0787 52 53 96 / 0717 086 135