Makala na Nassor Gallu
SIKU ya Agosti 8, mwaka huu kutakuwa na bonge la mechi litakalopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo wabunge wanaoshabikia Yanga, watakuwa dimbani kupepetana na wenzao wa Simba.
Hebu jaribu kuvuta picha katika ubongo wako, waheshimiwa wabunge watakapoweka kando masuala ya ‘Ukawa’ na ‘Tanzania Kwanza’, kisha kukutana katika uwanja kuonyeshana umwamba kwa kusakata gozi la ng’ombe katika mchezo huu wa kihistoria.
Kila timu tayari imeingia mafichoni kujiwinda na mchezo huo ili kuhakikisha inaibuka kidedea na kujenga heshima mbele ya watani wao huku Simba wakiahidi kulipiza kisago cha bao 1-0 walichokipata mwaka jana kutoka kwa Yanga.
“Tayari tumeingia kambini kujiwinda na mchezo huu ili kuziba midomo na kelele za Yanga ambao wamekuwa wakitamba tangu watubahatishe mwaka jana,” alijinasibu Hamis Kigwangala ambaye
ndiye nahodha wa Simba.
Kwa upande wa mlezi wa Yanga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abassi Mtemvu, alijigamba kuwa ni lazima waendeleze moto wa ushindi kwa kuwa wapo na kikosi imara na tayari wameshaingia kambini kwa kuwa mchezo huu ni siriazi kwao.
“Kwa kweli mchezo huu tumeuchukulia kwa mtazamo wa juu kabisa na lazima tuwapige kwa kuwa tuna damu changa nyingi, hatuna masihara, maana wakitufunga hatutakaa bungeni.
“Tupo katika maandalizi ya mwisho kwa sasa ingawa tulipoweka kambi yetu itabaki kuwa siri,” alisema Mtemvu kwa kujiamini.
Kila timu tayari imeingia mafichoni kujiwinda na mchezo huo ili kuhakikisha inaibuka kidedea na kujenga heshima mbele ya watani wao huku Simba wakiahidi kulipiza kisago cha bao 1-0 walichokipata mwaka jana kutoka kwa Yanga.
“Tayari tumeingia kambini kujiwinda na mchezo huu ili kuziba midomo na kelele za Yanga ambao wamekuwa wakitamba tangu watubahatishe mwaka jana,” alijinasibu Hamis Kigwangala ambaye
ndiye nahodha wa Simba.
Kwa upande wa mlezi wa Yanga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abassi Mtemvu, alijigamba kuwa ni lazima waendeleze moto wa ushindi kwa kuwa wapo na kikosi imara na tayari wameshaingia kambini kwa kuwa mchezo huu ni siriazi kwao.
“Kwa kweli mchezo huu tumeuchukulia kwa mtazamo wa juu kabisa na lazima tuwapige kwa kuwa tuna damu changa nyingi, hatuna masihara, maana wakitufunga hatutakaa bungeni.
“Tupo katika maandalizi ya mwisho kwa sasa ingawa tulipoweka kambi yetu itabaki kuwa siri,” alisema Mtemvu kwa kujiamini.
Wabunge wa timu ya Simba wakiwa kwenye picha ya pamoja. |
Baadhi ya wabunge wanaounda timu ya Yanga ni pamoja na Abassi Mtemvu, Ridhiwani Kikwete, Freeman Mbowe na Mwigulu Nchemba, huku kikosi cha Simba kikiundwa na wakali kama Zitto Kabwe, Hamisi Kigwangalla, Wiliam Ngeleja, Juma Nkamia, Amos Makalla na Ismail Aden Rage.
Mbali na mchezo huo ambao utakuwa kivutio kikubwa kwa wadau wa soka, pia kutakuwa na mchezo mwingine wa kusisimua pale Bongo Fleva chini ya mkali wao, Peter Manyika itakapopepetana na Bongo Movie FC chini ya Jacob Steven JB.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Bongo Movie, Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’, tayari ameanika wachezaji wake huku akisema kuwa hahofii kwani kikosi chake kipo kamiligado kuelekea mchezo huo ambao wameuchukulia kwa umakini mkubwa.
“Sisi tumeuchukulia ‘serious’ sana mchezo huu kwa kuwa mashabiki wetu watakuja wengi na hatutakubali kuwaangusha.“Wachezaji waliopo kambini mpaka sasa ni Mzee Majuto, Kingwendu, Bambo, JB, Steve Nyerere, Dk Cheni, Ray, Mtitu, Cloud pamoja na Muhogo Mchungu,” alisema Bi Mwenda.
Akijibu mapigo ya wapinzani wao, kocha wa Bongo Fleva ambaye pia anakinoa kikosi cha Yanga, Juma Pondamali ‘Mensah’, alisema Bongo Movie wajiandae kupata kipigo cha mshangao kwa kuwa wao hawatakwenda kuigiza uwanjani.
“Hawa waigizaji wajiandae na kipigo cha ‘sapraizi’, maana pale sisi hatuendi kuigiza, tunaenda kupiga kazi kwa kuwa mpira hauigizwi, unachezwa kila mmoja anaona, sasa acha wapige domo wataona kitakachowakuta,” alisema Pondamali.
Baadhi ya mastaa wanaounda kikosi cha Bongo Fleva ni pamoja na Peter Manyika, H-Baba, Ali Kiba, Rich One, Kalapina na wengineo.
Ukiachana na soka, pia kutakuwa na burudani mbalimbali ambapo mastaa kibao kutoka ndani na nje ya nchi watakuwepo kulipamba jukwaa la Usiku wa Matumaini.
Baadhi ya mastaa hao ni pamoja na Yemi Alade kutoka Nigeria, Madee, Ali Kiba, Roma Mkatoliki, Shilole, Menninah, Juma Nature na kundi zima la TMK Wanaume Halisi.
Mgeni rasmi katika tamasha hili atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal.Tamasha la Usiku wa Matumaini limedhaminiwa na Clouds FM (88.5), Times Fm (100.5), Vodacom, Pepsi, Azam TV pamoja na Syscorp.
MASTAA WAELEZA WATAKAVYOKAMUA TAIFA
ITAKUWA balaa! Siku chache kuelekea kwenye Tamasha la Matumaini, Agosti 8, mwaka huu, mastaa kibao watakaolipamba jukwaa litakalofungwa ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar, wameeleza jinsi gani
Yemi Alade
Diva wa muziki kutoka pande za Nigeria ambaye huwa habahatishi, amesema: “Nitawapagawisha mashabiki kwa kupiga nyimbo zangu zote kali ikiwemo iliyojizolea umaarufu kila kona ya Afrika, Johhny. Mashabiki wategemee kumuona Yemi akimaliza. Kati ya nyimbo ambazo nitazipiga ni Tangerine, Johnny, Bamboo, Birthday, Ghen Ghen Love na nyingine kibao.”
Ali Kiba
“Kwa mara ya kwanza, nitapanda jukwaa la Uwanja wa Taifa kuweka historia mpya. Mashabiki wengi ‘wamenimiss’, Agosti 8 itakuwa maalum kwa ajili yao. Wategemee ngoma kali kibao kutoka kwa mfalme wa Bongo Fleva niliyerudi kupangusa kiti changu na kukikalia, “Nitagonga kali kama Dushelele, Single Boy, Run Dunia na mpya zinazobamba kwa sasa ambazo ni Mwana na Kimasomaso.”
Shilole
“Mashabiki wategemee kuona shoo ya nguvu, hakuna anayebisha kwamba najua kuimba na kukitumia vyema kiuno changu. Nitazipiga Chuna Buzi, Paka la Baa, Nakomaa na Jiji, Lawama na hii mpya ya Namchukuwa.”watakavyolishambulia jukwaa.
R.O.M.A
“Huwa sibahatishi katika shoo zangu, nitawainua mashabiki kwa kunyoosha kidole cha mwisho juu kwa kupiga ngoma kali kibao kama Tanzania, Mechi za Ugenini, Pastor, Mr. President pamoja na hii mpya ya Karibu Kwenye Karamu (KKK).
Navy Kenzo
“Tutawapagawisha mashabiki kwa staili ya Bokodo iliyotokea kujizolea umaarufu mkubwa. Ngoma kama Cheza Kizembe, Usinibwage, Chelewa (Bokodo) na hii mpya ya Aiyola ndizo zitakazosisimua zaidi siku hiyo.”
Mkali wa Bongo Fleva, Juma Nature akipozi.
Juma Nature
“Huwa ushindi kwetu ni lazima, tutakamua Tatu Bila, Fitina, Nyama pamoja na ngoma mpya niliyomshirikisha Lady Jay Dee, Kama Jana.”
Scorpion Girls
“Sisi huwa hatubahatishi, unapomuona sehemu Isabela na Jini Kabula ujue timu nzima ya Scorpion Girls imetimia. Tutacheza na kuwaimbia nyimbo zetu kama Tanzania, Watuache na nyingine kibao.”
Madee
“Pale taifa nitakwenda kudhihirisha urais wangu wa Manzese, nitazipiga zote kali ikiwemo Pombe Yangu, Tema Mate Tuwachape na hii mpya ya Ni Shidaa, noma saaana!”
Meninah
“Nitawapagawisha kwa ngoma zangu kali kama Dream Tonight, Kacopy Kapaste na mpya ya sasa ambayo ni Pipi ya Kijiti. Tukutane pale taifa, Agosti 8 mwaka huu.”