Wasanii watengeneza filamu kuhusu Bunge la Katiba

Msanii Mohamed Jongo ‘Muddy Jongo’ aliyeandika muswada na kurekodi filamu kuonesha mwelekeo wa mawazo yaliyokuwa yakijadiliwa katika Bunge la Katiba lililofanyika mjini Dodoma, anatarajiwa kuiachia filamu hiyo mwezi ujao.

Kwa mujibu wa gazeti la TanzaniaDaima, filamu hiyo inaonesha unyonge wa wananchi, wabunge waliochaguliwa kuwawakilisha wanavyowadharau na kutaka kuweka kile wanachokitaka wao.

Pia, kwa jinsi michango ya mawazo ya wananchi isivyothaminiwa, Mzee Muungaro na wenzake kutoka Kijiji cha Amka wanajikusanya na kwenda Dodoma kunakofanyika vikao vya Bunge.

Baadhi ya washiriki katika filamu hiyo ni yeye (Jongo), Mzee Kibinda, Mikurupuko, Bibi Waiti, Mama Chambele, Mbega na Kindamba. Pia yumo mmoja wa wajumbe wa Bunge halisi la Katiba, Mama Jura.