"Watoto wa Kikwete" Taifa Stars watoshana nguvu na Msumbiji


Golikipa wa Stars, Deogratius Munishi akishangilia balo la pili la Taifa Stars kwa kuonyesha fulana yake iliyokuwa ikisomeka 'Sisi ni Watoto wa Rais Kikwete'.
Golikipa wa Stars, Deogratius Munishi akishangilia balo la pili la Taifa Stars kwa kuonyesha fulana yake iliyokuwa ikisomeka 'Sisi ni Watoto wa Rais Kikwete'.

Timu ya Taifa ya Tanzania leo imetoka sare baada ya kufungana bao 2-2 na timu ya Taifa ya Msumbiji katika mechi iliyokuwa na ushindani mkali mwanzo hadi mwisho katika kuwania nafasi ya kucheza katika kombe la Mataifa Africa 2015. 

Mabao ya Tanzania yamefungwa na mchezaji machachari Khamis Mcha yote katika dakika ya 65 na 71 kwa mkwaju wa penati huku magoli ya Msumbiji yakiwekwa kimiani na Elias Pelembe dakika ya 47 kwa mkwaju wa penati na Isack Carvalho dakika ya 87.

Mchezo ulikuwa mkali na timu zote zilishambuliana kwa zamu huku na mpaka kufikia mapunziko timu zote zilikua hazijafungana. Kipindi cha pili kilianza kwa Msumbiji kupata bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati na baadae timu ya Tanzania ilisawazisha bao hilo na kuongeza bao lingine lililopatikana kwa mkwaju wa penati na baadaye Msumbiji ikasawazisha zikiwa zimebakia dakika 3 mpira kuisha.

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Msumbiji katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Mbwana Samatta akiwatoka mabeki wa timu ya taifa ya Msumbiji. 




Mshambuliaji nyota wa Taifa Stars, Mbwana Samatta akiwa katikati ya mabeki wa timu ya taifa ya Msumbiji. 


Huniwezi...Mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akimtoka beki wa Msumbiji, Zainadine Junior. 
(picha zote: Francis Dande blog)