Yemi, Shilole kufanya maajabu katika Usiku wa Matumaini


WAKATI hamu ya mashabiki kila kona kwa sasa ni Agosti 8, mwaka huu katika tamasha kubwa la kihistoria la Usiku wa Matumaini litakalofanyia Uwanja wa Taifa jijini Dar, mashabiki wengi wanatamani kuwaona wakali kibao wakipanda jukwaani na kupiga nyimbo zao kali.


Diva wa muziki kutoka Nigeria anayetamba na wimbo wa Johnny, Yemi Alade

Good newz ni kwamba Zuwena Mohamed ‘Shilole’ atapanda jukwaa moja na diva wa muziki kutoka Nigeria anayetamba na wimbo wa Johnny, Yemi Alade kudondosha shoo ya kihistoria.

Uzuri wa wasanii hao wawili ndiyo unashawishi watu wengi kufika katika tamasha hilo lenye lengo ya kuchangia mfuko wa elimu nchini. Unataka kujua sifa za wasanii hao? Hizi hapa:

Shilole ambaye wengi wamezoea kumwita  Shishi Baby, amekuwa habahatishi jukwaani kwa jinsi anavyojua kuwapagawisha, hivyo mashabiki wategemee sapraizi kibao kutoka kwa bidada huyo kwenye sekta maalum ya kukata mauno na kuacha watu midomo wazi.

Kwa upande wake, Yemi Alade anatisha balaa. Staili ya Johnny ndiyo atakayoinesha siku hiyo huku akichungulia kwa kumtafuta Johnny uwanjani mpaka atakapofanikiwa kumuona na kurudi naye Nigeria kama alivyoahidi.

NGOMA ZAO
Pata picha kwa Shilole atapopanda na kupiga nyimbo zake kali kama Chuna Buzi, Lawama, Nakomaa na Jiji, Paka la Baa na Namchukua inayotamba kwa sasa, hakika patakuwa hapatoshi kwani Shilole amesema hatabakisha kitu siku hiyo.

Zuwena Mohamed ‘Shilole’

Bidada Yemi Alade atashuka na ngoma inayotamba Afrika, Johnny kisha atazidondosha kali nyingine ambazo zimetokea kuiteka Afrika kama GhenGhenLove, Bamboo, Show Me na Tangerine.

MADANSA

Shilole ameahidi kudondoka na madansa wake ambapo watakuwa naye sambamba jukwaani katika kukamua siku hiyo.

“Mashabiki wategemee kuona mpangilio na staili tofauti kutoka kwa masteji shoo hao ambazo zitakuwa funika bovu,” alisema Shilole.

Yemi naye hatakuwa nyuma katika eneo hilo, ameahidi kucheza sambamba na madansa wake siku hiyo. Kama ilivyo kwenye makamuzi yake kupitia video ya Johnny na Tangerine ambapo madensa wake wanaonekana wakikamua mwanzo mwisho.

WENGINE

Mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto amefunguka kuwa mbali na shoo hiyo kali, utamu zaidi utakolezwa zaidi na mastaa wakali wa Bongo Fleva wakiongozwa na mfalme, Saleh Ally ‘Ali Kiba’, Meninah, Madee, R.O.M.A Mkatoliki, Scorpion Girls, Juma Nature na kundi zima la TMK Wanaume Halisi.

“Kila msanii atakayepanda jukwaani atahakikisha anapiga nyimbo zake zote ndipo ampishe mwenzake, itakuwa ni jiwe baada ya jiwe,” alisema Maloto.

Aidha, tamasha hilo litapambwa na mechi za mpira wa miguu kati ya wabunge mashabiki wa Simba na wenzao wa Yanga, Bongo Fleva na Bongo Movie pamoja na mapambano kibao ya ndondi, burudani zote hizo mashabiki watazipata kwa kiingilio cha shilingi elfu tano.

Tamasha hilo limedhaminiwa na E.FM, Clouds FM, Times FM, Vodacom, Pepsi, Azam TV na SYSCORP.
JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS