Ajali nyingine ya mabasi yachukua uhai wa zaidi ya watu kumi


Watu wapatao 16 hivi wameripotiwa kupoteza maisha huku zaidi ya 70 wakiachwa na majeraha mbalimbali baada ya basi la Sabena lenye namba za usajili T 110 ARV likitokea Mbeya kwenda Mwanza na basi la AM Dreamline lenye namba za usajili T 803 ATN lililokuwa linatoka Mwanza kuelekea Mpanda kugongana uso kwa uso katika maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 4 to wilaya ya Sikonge.

Majeruhi waliwahishwa katika hospitali ya Mission ya wilayani Sikonge kwa matibabu zaidi.

Taarifa zinadai kuwa dereva wa basi la Sabena aliyefahamika kwa jina la James Kombe amepoteza maisha baada ya kukatika mwili na kufa papo hapo na kuwa jitihada za kutafuta kiwiliwili chake zilikuwa zikifanyika baada ya kupondeka vibaya.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa wasaidizi (day-worker).

.