Ajira za gesi Madimba ni za Watanzania

Mafundi wazawa wakiendelea na shughuli za ujenzi katika eneo panapojengwa kituo cha kuchakata gesi Madimba. Pichani mafundi wakishindilia mchanga kwa ajili ya kusawazisha eneo ambapo itafungwa mitambo mbalimbali katika eneo hilo.
Pichani ni baadhi ya nyumba ambazo tayari zimekamilika zitakazotumiwa na watumishi watakaofanya kazi katika kituo cha Kukachakata gesi Madimba. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Elikim Maswi, amesisitiza kuwa, shughuli mbalimbali katika kituo hicho zitafanywa kwa kiasi kikubwa na Wataalamu Watanzania.

Na Asteria Muhozya, Habari-Maelezo, Mtwara.

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imedhamiria kukifanya kituo unapojengwa mtambo wa kuchakata gesi cha Madimba kuendeshwa na wataalamu wa Kitanzania kwa asilimia kubwa.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho na kueleza kuwa, amefurahishwa na
kasi ya ujenzi wa kituo hicho jambo ambalo linaashiria mradi kukamilika katika muda uliopangwa.

Ameongeza kuwa, dhamira ya Wizara na Serikali ni kuhakikisha kuwa, wataalamu wazawa wa kitanzania wanapata ajira katika kila idara itakayohusika na shughuli za uchakataji gesi katika kituo hicho.

“Nataka niseme ajira za Madimba ni za watanzania. Wizara na Serikali inataka wataalamu wa kitanzania kufanya kazi katika kituo hiki, hilo liko wazi, wataalamu watanzania wapo na wanaweza,” amesisitiza Maswi.

Aliongeza kuwa, ili kuhakikisha kwamba watanzania wanapata ujuzi wa shughuli za gesi nchini, serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imekuwa ikiwatumia wataalamu wake kutoka hatua za mwanzo wa ujenzi wa mradi ili waweze kuendeleza shughuli hizo hata baada ya wakandarasi na wataalam kutoka makampuni mbalimbali yanayofanya shughuli za ujenzi wa miundombinu ya mradi huo kuondoka.

Mafundi wakiziba mabomba ya gesi kabla hayajafukiwa ardhini kwa ajili ya kusafirisha gesi katika eneo la Msijute Mtwara. Kwa mujibu wa Mhandisi Kapuulya Musomba, kabla ya mabomba ya gesi hayajafukiwa ardhini hufanyiwa 'testing' kasha sehemu zenye dosari huzibwa kabla ya kufukiwa ardhini.
Aidha, Maswi amesisitiza kuwa, serikali imejipanga kuhakikisha kwamba kupitia sekta ya gesi na mafuta nchini Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi zenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 na kuongeza kuwa, jambo hilo linawezekana.

Kwa upande wake Meneja Mradi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba ameeleza kuwa, kiasi cha gesi kitakachozalishwa nchini kutaliweka vizuri Shirika la Umeme Tanzania kuwa katika halinzuri ya kuzalisha umeme kutokana naTanzania kuwa na kiasi kikubwa cha gesi kilichovumbuliwa.

“Gesi tunayo nyingi sana, mnazi gesi imekaa tangu mwaka 1985 haijachimbwa, uhakika wa nishati kwa Tanzania upo”, amesisitiza Musomba.

Ameongeza kuwa, TPDC imefurahishwa na ushirikiano mzuri kutoka serikalini na kutoka Wizara ya Nishati na Madini ambao kwa kiasi kikubwa umewezesha mradi huo kufika katika hatua hiyo kubwa.

“Mwanzo ulikuwa mgumu lakini sasa tuko vizuri sana tunakwenda kama tulivyopanga. Bila msaada wa Wizara na Serikali tusingefika huku. Namshukuru sana Katibu Mkuu kwa kulifanikisha hili,” ameongeza Musomba.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (wa kwanza kushoto) akiangalia madini aina ya ‘gypsum yanayochimbwa na Kampuni ya Kwanza Kilwa. Eneo la Kiranjeranje Mtwara. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mohamed Gani. Wa kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi Kanda ya Kusini, Mhandisi Benjamin Mchwampakaka.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (wa kwanza kushoto) akiangalia madini aina ya ‘gypsum yanayochimbwa na Kampuni ya Kwanza Kilwa. Eneo la Kiranjeranje Mtwara. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mohamed Gani. Wa kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi Kanda ya Kusini, Mhandisi Benjamin Mchwampakaka.

TUTATOA LESENI ZA MADINI KWA WACHIMBAJI MAKINI


Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi ameeleza kuwa, Wizara itawapatia leseni wachimbaji madini makini wanaoendeleza maeneo yaonakwa wale wasioyaendelea ndani ya kipindi cha miaka saba watanyanga’nywa.

Katibu Mkuu Maswi ameyasema hayowakati wa ziara yake Lindi hapa alipotembelea shamba la kuzalishachumvi eneo la Mshindo linalomilikiwa na familia ya Said Tamimu nakuongeza kuwa, ziara yake imelenga kutembelea miradi inayotekelezwa na wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na kutaka kufahamumatatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo wachimbaji hao.

“Ukiangalia, tayari kuna leseni zaidi ya 1000 za madini ambazo zimetolewa Mtwara lakini wanaoendeleza maeneo yao ni wachache. Kwa hivyo sisi tutaendelea kuwakagua na kwa wasiyoyaendeleza ndani ya kipindi hicho tutawanyanga’nya,” amesisitiza Maswi.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi Kanda ya Kusini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, ameeleza kuwa, Serikali iko tayari kuwasaidia wachimbaji wadogo ambao wanafanya shughuli zao vizuri na zenye mafanikio na hivyo itaendelea kuwawezesha ili wawezekupata mikopo na ruzuku za kuendeleza shughuli zao.

“ Mzalishaji huyuameonesha mfano mzuri kwa kuwa mzalishajimkubwa wa chumvi, hivyo serikali itahakikishawawekezajina wachimbaji wazawa kama hawa wanapata ruzuku au mikopo ili waweze kununua mashine za kumwezesha kuzalisha zaidi na hivyo kuongeza thamani katika bidhaa zao;” amesisitiza Mchwampaka.

Kwa upande wake Said Timamu meneja wa kampuni ya uzalishaji chumvi, ameleza kuwa, endapo serikali itawawezesha wazalishaji na wachimbaji watakuwa katika nafasi nzuri ya kuzalisha zaidi na kuongeza thamani ya madini wanayozalishahivyo kuiwezesha serikali kupata kodi inayostahili kutokana na madini wanayoyazalisha.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu ametembelea wachimbaji wa madini aina ya gypsum katika eneo la Kiranjeranje na kupata fursa ya kuonana na mkurugenzi wa kampuni ya Kwanza Kilwainayochimba madini hayo, Mohamed Gani ambapo pia amesisitiza suala la kuendeleza maeneo yao na umuhimu wa kufuata sheria za uchimbaji madini kwa wamiliki kwawa leseni za uchimbaji.