Ambaka mtoto wa mwaka mmoja u nusuMtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu mkazi wa Sokoni One jijini Arusha, amebakwa na kunajisiwa na mwanamme mwenye umri wa miaka 30.

Mama wa mtoto huyo, Mwitango Yambazi Mtalu (27),  alisema siku ya Jumapili majira ya asubuhi alimkabidhi mtoto wake kwa jirani yake aliyemtaja kwa jina la Mustafa Kabananga, ili apate nafasi ya kushiriki mkutano wa kikundi chake.

Ilidaiwa kuwa mtuhumiwa aliyetajwa kwa jina la Rajabu Mkoba, mkazi wa eneo hilo, alimchukua kutoka kwa mtu huyo aliyepewa kumtunza, kisha akambaka mtoto huyo kwa zaidi ya saa 9.

Tukio hilo lilitokea Agosti 3 mwaka huu.

Mama mzazi wa mtoto huyo hakutoa taarifa polisi baada ya kuahidiwa shilingi 100,000/=
“Nilikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa, yeye anaishi na wazazi wake. Hata hivyo, sikumkuta mwanangu wala mtuhumiwa, nikarejea nyumbani. “Lakini kabla sijarudi, nilimwambia mama wa mtuhumiwa kuwa mwanaye kaondoka na mtoto wangu akaniambia nirudi nyumbani nikaendelee kumtafuta nikimkosa niende kwake ili akajue cha kufanya, aliamua kwenda polisi’ “Ilikuwa saa 9 usiku nikiwa narejea nyumbani kutoka polisi, nilimkuta mama mzazi wa mtuhumiwa akiwa na mtoto wangu akimrejesha kwangu lakini mtuhumiwa hakuwepo.“Niliamua kumchunguza vizuri mwanangu ndipo nilipogundua kuwa sehemu zake za siri zimevimba kupita kiasi huku damu zikimtoka.
“Nilikwenda kumweleza mama yake jinsi mwanaye alivyomtenda mtoto wangu na kumwachia mtoto ampeleke hospitali, alinisihi nisitoe taarifa za tukio hilo popote na akaniahidi kunipa shilingi laki moja,” 

alisema mama huyo.

Imeelezwa kuwa mama wa mtuhumiwa baada ya kukabidhiwa mtoto huyo hakumpeleka hospitali badala yake alikuwa akimtibu kwa kutumia miti shamba.Baadhi ya majirani walikerwa na kitendo cha mwanamke huyo ambapo walimvamia na kumtolea maneno makali ya kumtaka alifikishe suala hilo kwenye vyombo vya sheria.

Kufuatia kelele za majirani ndipo alipokubali kurudi Kituo cha Polisi cha Unga Ltd ambapo polisi walifika nyumbani kwa mama wa mtuhumiwa na kumchukua mtoto huyo kisha kumwandikia hati ya matibabu (PF3) na kumpeleka mtoto huyo katika Hospitali ya Mount Meru ambako anatibiwa.

Polisi hao walifungua jalada la mashtaka la kubaka na kunajisi lenye namba Ung/RB/2473/2014, bado mtuhumiwa hajakamatwa kwani alikimbia baada ya tukio hilo lakini mama yake ameshikiliwa kwa mahojiano.
-- Joseph Ngilisho, Arusha,