![]() |
Watoto wakisakata kabumbu huko Malindi Kenya kama walivyonaswa na kamera mwaka 2010 (picha: dreamstime.com) |
Pamoja na sheria 17 za soka za FIFA kuwepo, enzi za utoto kulikuweko na sheria za soka ambazo ndizo zilizokuwa zinatambuliwa:-
- Mwenye mpira ndiye anayeamua nani atacheza
- Mtoto bonge ndiye golikipa
- Wachezaji mahiri ndio wanaochaguliwa kwanza
- Kukiwa na penati ruksa kubadilisha kipa
- Ukipiga mpira kwa nguvu au kwa mandochi mwenye mpira ana ruhusa ya kukuonya au kukukataza usicheze
- Usipochagia hela ya kujaza upepo utapigwa marufuku kucheza
- Hakuna marefa wala malinzmeni, na mpira unachezwa mpaka kuzunguka goli
- Kumkaba mwenye mpira faulo
- Ukitoboa mpira unalipa
- Mwenye mpira akikasirika au akiumia au akiitwa na mama yake ndio mwisho wa mechi
Imetoka kwa uncle John Kitime. Mtembelee kwenye blogu yake kwa vichekesho zaidi chekanakitime.blogspot.com