Picha zaidi zimepachikwa hapo chini pamoja na audio na video...
Watanzania waishio Ughaibuni wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete wakati wa kongamano la Watanzania waishio ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini leo Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete akiangalia tovuti ya Taasisi ya Watanzania waishio Ughaibuni ya baada ya kuizindua tovuti hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watanzania waishio Ughaibuni wakati wa kongamano la Watanzania waishio ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini, leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na audio: Habari/Maelezo