Dar es Salaam, Agosti 11, 2014:
Bia maarufu ya Castle Lite, inayozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imezindua rasmi promosheni ya aina yake itakayojulikana kama “Lite Up The Weekend”. Promotion hii ya aina yake hapa nchini itadumu kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Agosti hadi Octoba 2014.
Akizungumza katika uzinduzi huo, meneja wa Bia ya Castle Lite Geoffrey Makau alisema; Bia ya Castle Lite kwa mara nyingine tena inawaletea wapenzi wa bia hii habari nzuri na za kuvutia. Leo tunazindua promosheni kubwa itakayojulikana kama “Lite Up The Weekend”.
Hii ni promosheni kubwa itakayoendeshwa nchi nzima. Washindi watashiriki kwenye hii promosheni kupitia chupa za bia ambazo watatakiwa kutuma nambari ya siri iliyochini ya kizibo cha bia ya
Castle Lite.
Tumewaandalia wateja wetu zawadi mbalimbali zitakazokuwa zikitolewa kila wiki, ikiwa ni pamoja na zawadi za pesa taslimu, zawadi za vifaa vya kusikilizia muziki (headfone) n.k, lakini zawadi kubwa zaidi ni ile ya washindi kupata fursa ya kusherehekea kwenye VIP Party ndani ya Boti ya kifahari. Sherehe hii itajulikana kama “Castle Lite VIP Yacht Party”
Mteja atatakiwa kununua bia ya Castle Lite ya chupa yenye ujazo wa mililita 375 au 330 na kuangalia chini ya kizibo cha Bia, ambapo atakuta namba za siri, kisha atatuma namba hizo kwenda 15499 au kutembelea website yetu ambayo ni, www.castlelite.co.tz, ili apate nafasi ya kushinda zawadi za kila wiki au zawadi kubwa ya “Castle Lite VIP Yacht Party”.
Washindi wa zawadi kubwa kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania, watapata fursa yakuparty na wenza wao kwenye boti la kifahari aina ya yacht, ambayo itaondoka Dar kuelekea kisiwa kizuri kilicho andaliwa kwa ajili yao, huku wakiburudishwa kwa chakula, vinywaji na muziki.
Promosheni hii pia itapewa msukumo mkubwa kupitia Radio, ambapo wapenzi wa Castle Lite watapigiwa simu na watatakiwa wapokee kwa kuanza na neno ya “Lite Up My Weekend”. wateja watakaofanya vizuri watapata zawadi mbalimbali kila wiki. Alisema Makau.
Zaidi ya zawadi za kila wiki, wateja pia watashinda nafasi za kuhudhuria matamasha mbalimbali yanayoambatana na muziki hapa nchini. Ninawaomba sana wapenzi wa bia hii ya Castle Lite, kushiriki mara nyingi iwezekanavyo ili kushinda zawadi hizi za kuvutia, aliongeza Geoffrey.
![]() |
Wanahabari wakielekea eneo la maegesho ya Yacht itakayotumika katika kilele cha cha kampeni ya Lite Up The Weekend. |
![]() |
Muonekano wa Yacht itakayoandaliwa maalum kwa ajili ya washindi wa shindano la Lite Up the weekend. |
![]() |
Mmoja ya wadau wadau wa Castle Lite katika pozi ndani ya Yacht. |
![]() |
Meneja masoko wa Castle Lite Vimal Vaghmaria na Stanley Kafu wa Aggrey & Clifford wakifurahia ndani ya Yacht. |
-MWISHO-
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:
Geoffrey Makau – Castle Lite Brand Manager, +255767266513, [email protected]
Kuhusu TBL
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) ni watengenezaji na wauzaji wa bia safi, vinywaji vyenye virutibisho na vinywaji visivyo la kilevi nchini Tanzania. TBL pia ina hisa katika Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) na Darbrew Limited.Vinywaji maarufu za TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lite, Castle Lager, Castle Milk Stout, Redd’s Original, Peroni Nastro Azzurro, Balimi Extra Lager, Eagle Lager, Eagle Dark, Club 07, Vita Malt, Grand Malt and Safari Sparkling Water. Bidhaa nyingine ni Konyagi Gin na Zanzi Cream Liqueur.
TBL pia imo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam. Imeajiri watu wapatao 1,700 na ina wawakilishi kote nchini Tanzania ikiwa na viwanda 4 vinavyotengeneza bia safi, kitengo cha bia ya asili, kiwanda cha kusindika kimea na vituo vya mauzo 10. TBL ambayo ni kampuni inayoongoza katika uzalishaji wa vinywaji venye kilevi na visivyo na kilevi, imejitika kwenye kusambaza bidhaa zake kwenye masoko makubwa ndani na nje ya nchi chini ya makubaliano ya kufanya biashara chini ya soko la pamoja la jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kuhusu SABMiller
SABMiller plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabara matano. Bia zake ni pamoja na zile za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji nchini India.SABMiller imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya London na Johannesburg.