Bomba la mafuta, TAZAMA latobolewa Gongo la Mboto; Wananchi wateka mafuta yaliyotiririka mtaroni

Mafuta hayo yakitiririka katika mtaroni mithili ya maji.

Na Father Kidevu blog - Bomba la mafuta linalotumika kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Dar es Salaam Tanzania hadi Nchini Zambia lijulikanalo kama TAZAMA limetobolewa na mafundi wa Kampuni ya Raddy Fiber Solutution Ltd ya jijini Dar es Salaam wakati wakichimba chini ya barabara kupitisha awamu ya pili ya kebo za mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika eneo la Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

Picha zaidi...


Sehemu inayoonesha mafuta ya kimiminika baada ya bomba hilo kutobolewa chini.

Meneja Mkuu wa kampuni ya Raddy, Rajab Mikumwo amesema mafundi wake walitoboa bomba hilo kwa bahati mbaya majira ya saa nane alasiri leo wakati wakifanya kazi ya kuchimba njia ya kupitisha bomba.


Wakazi wa Gongo la Mboto wake kwa waume wakiwa katika pilika za kuchota mafuta hayo machafu ya dizeli.


Mkazi wa Goms akiondoka na dumu lake la mafuta.