Bunge la Katiba lapitisha Azimio la Mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni

Bunge Maalum la Katiba limepitisha Azimio la Mapendekezo ya Marekebisho ya baadhi ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba ili kuwezesha ili kuwezesha kujadili Rasimu ya Katiba kwa muda wa siku 60 za nyongeza na tatu zilizobakia.

Marekebisho hayo yamepitishwa kufuatia Mwenyekiti wa Kanuni na Haki za Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Pandu Ameir Kificho kuwasilisha mapendekezo ya kanuni hizo mapema leo asubuhi katika Bunge hilo mjini Dodoma mara baada ya kuanza kikao cha 30.

Azimio hilo limepitishwa baada ya baadhi ya wajumbe kuchangia hoja hiyo na kuungwa
mkono, ambapo uamuzi huo ulitangaza na Mwenyekiti wa Bunge hilo Mhe. Samuel Sitta.

Mhe . Sitta alisema Bunge hilo, litaanza kujadili sura zote za Rasimu ya Katiba Mpya katika kamati 12 kuanzia kesho tarehe 6 Agosti, mwaka huu kwa muda wa siku 15 yaani hadi Agosti 27, mwaka huu.

“Hivi sasa watumishi wa Bunge na Sekretarieti wanaweka nyezo zote za kupitia , ambapo pia Katibu wa Bunge Maalum la Katiba yupo nao anashughulikia suala hili pamoja na kamati ndogo ili kuwezesha kazi hii kufanyika bila buguza,” 
alisema Mhe. Sitta na kuongeza kwamba baada ya hapo kutakuwa na siku tatu kwa kamati kukamilisha Rasimu zao za Katiba.

“Kamati zinatakiwa kutumia sekretarieti ndogo kuandika sura wasisubiri hadi Agosti 28, mwaka huu. Tumeongeza idadi ya wataalamu katika kila sekretarieti ndogo,” 

Aidha Mhe. Sitta alisema kutokana na marekebisho ya Kanuni ya 32 kifungu cha 2 kinachosema kamati kubadilisha sura za rasimu na sura, hivyo zinatakiwa kutumia muda wa siku saba kupendekeza sura mpya kuanzia Agosti 6,mwaka huu hadi Agosti 13,mwaka huu.

Akizungumzia kuhusu maudhurio ya wajumbe wa Bunge hilo, alisema watakiwa kutia saini kwenye maudhurio hayo na hakuna kusainiana kila mtu atatia saini mwenyewe.

Mhe .Sitta akifafanua kuhusu utaratibu wa kutoa taarifa za kamati kwa vyombo vya habari alisema utatolewa.

Alisema Bunge hilo litarejea Septemba 2, mwaka huu baada ya kukamilisha kazi za kamati.

Bunge hilo limeanza vikao vyake kwa mara nyingine leo, baada ya kuairishwa Aprili 25, mwaka huu.

---
Imeandikwa na Magreth Kinabo via Tz Govt blog