Mfanyakazi wa maabara ajionyonga hadi kufa


* Taarifa hii imerekebishwa baada ya kupatikana taarifa sahihi zaidi.

Mfanyakazi wa maabara aliyestaafu mwezi Aprili mwaka huu katika Hospitali ya Mtakatifu Joseph ya Peramiho amejinyonga.

Mwili wa marehemu umekutwa uking’inia leo asubuhi kando ya uwanja wa mpira wa miguu wa Peramiho, Songea Vijijini.

Marehemu ameacha ujumbe kwenye kijikaratasi kilichokutwa mwilini mwake kilichoeleza kuwa amefikia uamuzi wa kuondoka dunia kutokana na ugomvi wa muda mrefu kati yake na mkewe na
kuelekeza kuwa baada ya kuondoka kwake duniani mkewe aondoke kwenye nyumba yake na arudi kwao Msamala, mjini Songea.

Watu waliokuwepo katika eneo la tukio wamekiri kuwa marehemu na mewe wamekuwa katika ugomvi wa muda mrefu uliosababisha wafikishane katika vyombo vya kisheria mara kadhaa japo kuwa hakuna aliyeeleza ugomvi huo ulisababishwa na nini.

Tayari Polisi wameuchukua mwili wa Marehemu kutoka eneo la tukio na kuuhifadhi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Peramiho.

DemashoNews - DAKTARI MSTAAFU WA HOSPITAL YA PERAMIHO AJINYONGA
DemashoNews - MFANYAKAZI WA HOSPITALI YA PERAMIHO SONGEA AJINYONGA