Fununu ya 'mlungula' yasababisha CHADEMA Geita watiane adabu


Wafuasi wa CHADEMA wakitaka kuzichapa nje ya Wandela hotel mjini Geita katika tukio la wanachama chama hicho kukutwa kwenye kikao cha siri katika hotel ya Wandela iliyopo Shilabela mjini Geita, ambapo kwenye kikao hicho ilidaiwa walikuwa wanagawiwa mlungula ili kupitisha kambi ya Katibu wa CHADEMA jimbo la Geita Rogers Luhega ambaye yuko taabani kisiasa dhidi ya mpinzani wake Mutta Robert aliyeomba kugombea nafasi hiyo.

Wanachama wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilayani Geita wamenusurika kutwangana makonde baada ya wenzao,wakiwemo viongozi wa matawi zaidi ya 50 kukamatwa na vijana wa ulinzi wa chama hicho (Red Brigade) wakiwa katika hoteli ya Wandela mjini Geita wakiwa kwenye kikao cha siri na kudaiwa walikuwa wanapokea rushwa kutoka kwa wagombea.

Kundi hilo la siri linadaiwa kuandaliwa na katibu wa Jimbo la Geita aliyepo sasa hivi Rogers Ruhega ikiwa ni mkakati wa kumuwezesha kurudi madarakani katika uchaguzi unaokuja ambao inaonekana ameelemewa na mgombea mwenzake Mutta Robert.

Ruhega ambaye hakuwepo katika kikao hicho, inadawa wajumbe waliokutwa Hotelini hapo ni kundi lina lohaha kila siku kutaka arudi madarakani kwa gharama yoyote na moja ya mbinu walizokuwa wanatumia ni kuchafua mgombea mwenzake na na kutoa rushwa.

Mgombea wa nafasi ya ukatibu wa Jimbo Mutta Robert ambaye alifika katika eneo la tukio alisema kuwa anatafakari hatua za kuchukua kulingana na kanuni za uchaguzi za chama
“Leo tumejaza fomu mpya za kugombea uongozi zinazoonyesha kanuni na maadili ya mgombea wakati wa uchaguzi ndani ya chama,yote haya yaliyotokea hapa leo ya kununuliana chakula,vinywaji na vikao vya siri vimekatazwa, hivyo natafakari, baada ya siku chache nitajua nichukue hatua gani za kikanuni kulingana na taratibu za chama maana ushahidi tayari ninao mkononi”

“Nilipogombea nafasi hiyo ya ukatibu wa Jimbo nilizushiwa mambo mengi mabaya ili kudanganya wajumbe ambao ni wapiga kura ili wasiniamini, na kashfa nyingi dhidi yangu lakini nilijipa moyo kwamba ukweli utajulikana nani ni mla rushwa au mtoa rushwa au nani anakiuka kanuni za CHADEMA”

Kundi hilo la wanachama zaidi ya 50 lilialikwa na mwanachama mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Wambura kwa lengo la kuweka mikakati ya kushinda katika uchaguzi unaoendelea ndani ya chama hicho katika ngazi ya Jimbo.

Katibu wa Jimbo Rogers Ruhega anayetuhumiwa kuandaa kikundi hicho,alipotafutwa simu yake haikupatikana,mbali na kuwa amekuwa akikana tuhuma hizo kwenye vyombo vya habari.

Hata hivyo taarifa zilisema kuwa alikuwa na kikaokingine cha siri viongozi wa kata ya Mtakuja ili kuweka utaratibu wa uchaguzi wa jimbo kinyume cha kanuni za chama hicho.

Katibu huyo anadaiwa kuwatumia baadhi ya viongozi wa chama hicho wa ngazi mbalimbali ili kumtengenezea mazingira ya kurudi madarakani,wanaotajwa kuratibu mkakati huo ni Mratibu wa Vijana mkoa Neema Stephen aliyekutwa ukumbini hapo na katibu wa Bavicha Jimbo la Geita Ngurubrighjt Tanganyika.

Viongozi hao wawili wanadaiwa kuzunguka katika kata mbalimbali za jimbo hilo waliongea na viongozi wa kata na kumkashfu Mutta Robert kwamba ametumwa na ccm na amepewa milioni 30 ili kuibomoa chadema ikiwa ni mbinu chafu za kuwatisha wapiga kura wasmchague.

Tukiola kukamata wanachama hao wakidaiwa kupewa rushwa na viongozi hao limekuja siku tatu baada ya Kamati tendaji ya Jimbo la Geita kutengua uongozi wa kata ya Kalangalala kwa kisingizio kwamba uchaguzi wake ulikiuka katiba,madai ambayo yalisemekana sio kweli ila Katibu wa Jimbo alishawishi kamati tendaji kuvunja uongozi huo baada ya kugundua viongozi wengi wa kata hiyo wanamuunga mkono mgombea mwenzake katika mchakato wa uchaguzi wa Jimbo.

Vijana hao ambao ni walinzi wa chadema walikuwa wameongoza na waandishi wa habari watatu na kufanikiwa kuwapiga picha wakiwa ukumbini hapo huku wakikutwa na vinywaji vya aina mbalimbali kama soda maji ,juisi na wachache walikuwa wanakunywa bia.

Mwenyekiti wa Baraza la vijana tawi la mkoani Baraka Cosmas alikiri kwamba aliitwa kwenye kikao hicho na Ngurubright Tanganyika na Neema Chozaile ili kuweka mikakati ya ushindi wa uchaguzi wa hivi karibuni.

Naye Michael Kalekwa ambaye ni kiogozi wa kwanza wa chadema katika jimbo la Geita aliseyekuwemo katika kikao hicho alisema kuwa kikao hicho sio cha kikatiba bali alipata mwaliko na alipofika aliuliza kama viongozi ngazi ya Jimbo wa nakifahamu kikao hicho akajibiwa Katibu wa Jimbo anajua kila kitu.

Aliyekuwa mwenyekiti wa kikao hicho cha siri,Nchegwa Nchegwa ambaye pia ni mwalimu wa sekondari ya Nyankumbu alisema kuwa kikao hicho ni halali kikatiba japo alipoulizwa kutaja cheo chake kilichomuwesha kuitisha kikao hicho alimtaka mwandishi kuandika aonavyo.


Red Brigades wavamia hotel na kukuta wenzao wanajichana kwa soda na maji kabla ya timbwili

 
Red Brigades wakiwa nje ya hotel wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini

 Baada ya kuvamia hapo ni nje ya ukumbi ngumi nje njecredit: Picha na Taarifa ya Victor Bariety via Malunde1 blog, Geita