Hali halisi ya maisha katika upande mwingine wa IrakWapiganaji takriban 5,000 wa kabila la Kurd kwa kutumia magari ya ujenzi yenye vijiko, matrekta, malori pamoja na punda wamesindikiza katika sehemu salama kiasi mamia ya wakimbizi wa kabila la Yazidi nchini Irak waliokwama kwenye milima wakiwa wamezingirwa pande zote na kundi linalodai kuanzisha taifa la Kiislam, la ISIS (Islamic State of Irak and Syria). 

Baadhi ya watu wa kundi hilo la kabila ndogo la Yazidi, walilazimika kuondolewa eneo hilo kwa miguu, wakipitia kwenye jangwa.

Bado kuna maelfu ya watu waliokwama katika maeneo hatari kwenye mlima Sinjar.