NMB inashiriki maonyesho ya wakulima ya nane nane katika mikoa saba huku huduma zote za kibenki zikiwa zinafanya kazi katika mabanda yake kama kuweka na kutoa fedha, kupata taarifa za mikopo hasa ya kilimo.
NMB inashiriki maonesho ya Nane Nane katika mikoa ifuatayo; Lindi ambako yanafanyika kitaifa, Morogoro, Dodoma, Tabora, Mbeya, Arusha na Kagera.
Wakulima pia wanaotembelea mabanda ya NMB kote nchini watapata fursa ya kukutana na wataalam wa kilimo na pembejeo, vyama vya ushirika na hivyo kuwa na fursa nzuri za wao kupata taarifa sahihi na ushauri wa jinsi ya kutumia benki kunufaisha shughuli zao za kilimo.
Kwa kuwa moja ya malengo ya NMB ni kuhakikisha inasaidia ukuaji wa kilimo na kukifanya kuwa cha kibiashara, yenye malengo la kumkwamua mkulima. Hii ni fursa nzuri kwa wakulima, wafanyakazi wa serikali na wajasiriamali kuweza kufika kwenye mabanda ya NMB ili kujionea huduma ambazo benki inatoa.
Kilimo ni uti wa mgongo kutokana na ukweli kwamba karibia 80% ya watanzania wanajishughulisha na kilimo. Kwa kutambua hilo, NMB ipo karibu yao zaidi katika kipindi hiki cha Nane Nane kwa kuleta huduma za kuwanufaisha.
Kauli mbiu ya ‘Kilimo na Mifungo ni biashara’ kwa mwaka huuimeifanya NMB kushirikiana na serikali katika kufanikisha maonyesho ya nane nane katika mikoa yote saba.
Benki ya NMB inatoa huduma mbali mbali za kilimo ikiwa ni pamoja na akaunti maalumu ya Kilimo yaani ‘Kilimo Account’ ambayo inamruhusu mkulima kuweza kujipatia mikopo mbali mbali ili kuweza kuinua uchumi wa Nchi.