Katiba inayotafutwa ni ya CCM na siyo ya Tanzania - Prof. Baregu

Akizungumza na NIPASHE jana, aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,  Prof. Baregu, aliliomba radhi taifa yeye binafsi na kwa niaba ya wenzake 30 waliokuwa kwenye Tume hiyo, ambao kati yao hiyo 15 kutoka Tanzania Bara na 15 Zanzibar, kwa kutekeleza mchakato wakiamini ni wenye lengo la kupatia Taifa Katiba mpya, kumbe walilaghaiwa wakatumika kuitumikia CCM kutafuta Katiba yake.
“Niligoma kujitoa kwenye Tume nilipotakiwa kufanya hivyo na chama changu (CHADEMA), nikiamini mchakato ulikuwa kwa maslahi ya taifa, kumbe tulilaghaiwa na sasa binafsi nimeamini Katiba inayotafutwa ni ya CCM na siyo ya Tanzania”
Prof. Baregu alisema uamuzi wa CCM wa kubariki Bunge Maalum la Katiba liendelee siyo wa busara wala hekima bali umegubikwa na mihemko ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Kwa mujibu wa Prof. Baregu, kinachoelezwa na chama tawala kuwa kuna maendeleo mazuri katika mchakato wa Katiba, ni kuondoa mambo yote yaliyo kwenye Rasimu ya pili, ambayo yalilenga kudhibiti nidhamu, uwajibikaji na utumishi bora kwa umma.
“Mgawanyo wa majimbo, ukomo wa mtu kugombea ubunge, miiko na maadili ya watumishi wa umma na mawaziri kutotokana na wabunge, vyote hivyo wanaviondoa kwenye rasimu wanataka kuunda utumishi au uongozi wa aina gani kama siyo unafiki?” “Hatunabudi kuomba radhi Watanzania tuliowaahidi kuwaletea Katiba Mpya.”
amenukuliwa Prof. Baregu akisema hayo.

NIPASHE - Baregu:Najuta