Akizungumza na NIPASHE akiwa mjini Dodoma, ambako vikao vya Bunge hilo vinaendelea, Dovutwa alisema wajumbe hao wana haki na uhuru wa mawazo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aliwashauri wasichoke wala kupumzika na badala yake waendelee kushikilia msimamo wao wa kushinikiza Bunge lisitishwe kwa nguvu zao zote hadi mwisho ili kuona wanapata kile wanachotarajia.
“Nawashauri wasitetereke, wasiogope, wasimame hapo hapo walipo maana wana haki ya
kufanya hicho wanachokifanya, wako sahihi kabisa, rasimu ikitoka kwa ajili ya kupigiwa kura waipinge na hata katiba mpya ikipita waipinge pia maana ni haki yao,”
alisema Dovutwa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha UPDP.
Alisema hakuna cha ajabu kwa vyama vingine vya siasa kugomea mchakato huo wa katiba wakati vyama vingine vikiendelea kwa kuwa uzoefu wa miaka ya nyuma unaonyesha kuwa huo ni mwendo wa kawaida kwa wapinzani kutofautiana misimamo.

“Mwaka 1995 tulipopata kugomea Uchaguzi Mkuu tukitaka mabadiliko ya katiba, wenzetu NCCR-Mageuzi walikataa, mwaka 2000 tukasema tugomee uchaguzi CUF ikakataa inasema haiwezi kumwachia nguruwe shamba, mwaka 2005 tulipoigomea Tume ya Jaji Lewis Makame, wenzetu CUF na Chadema walikutana na CCM kwenye hoteli moja hivi wakazungumza wakabadili msimamo wao, sasa leo hii haiwezi kuwa kitu cha ajabu sisi tuko ndani wao wako nje ya Bunge,”
alisema Dovutwa.
Alisema hata mwaka 1998 vyama vya upinzani viligoma kupeleka maoni yao kwenye tume ya Jaji Robert Kisanga, lakini wenzao wa CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi waliwageuka na kuwasilisha maoni yao kwa tume hiyo.

“Wao waendelee na msimamo wao ila sisi tutabaki bungeni, katiba ipatikane, isipatikane sisi wengine tutaendelea kuhudhuria maana kutofautiana ni jambo la kawaida kabisa katika siasa,”
alisisitiza Dovutwa.
via NIPASHE