Kesho kuna Mkutano wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wanahabari

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Fredrick Werema atazungumza na Wanahabari kesho, Jumamosi, Agosti 16, 2014 kuanzia saa 4:30 asubuhi katika Ukumbi wa Mikutano (Ground Floor) wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora uliopo katika Jengo la Haki (Haki House), mtaa wa Luthuli -- mkabala na jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais na mita chache kutoka Makao Makuu ya Wizara ya Fedha.

Katika mkutano huo, Mhe. Jaji Werema atafafanua masuala kadhaa ya kisheria yanayohusu mchakato wa Katiba.

Nyote mnakaribishwa. Wanahabari mnaombwa kuwa ukumbini ifikapo saa 4:15 asubuhi kesho.