Kuhusu taarifa za kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola nchini Tanzania


Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya na Ubora, Dk.Fausta Mosha (kulia), akitoa ufafanuzi wa kimaabara kuhusu ugonjwa huo.
Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya na Ubora, Dk.Fausta Mosha (kulia), akitoa ufafanuzi wa kimaabara kuhusu ugonjwa huo.

Baada ya kuenea kwa taarifa kuwa kuna watu wawili, mmoja raia wa nje na mwingine Mtanzania kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola, serikali imethibitisha kuwa hadi sasa hakuna mgonjwa wa Ebola nchini. Imesema wagonjwa waliohisiwa awali, walikuwa na magonjwa tofauti.

Akizungumza leo asubuhi na kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio, Waziri wa Afya, Dk. Seif Rashid amesema wagonjwa hao waliohisiwa kupata maambukizi kutokana na dalili za awali, ni wa kutoka Benin na Mtanzania.

“Kuna wagonjwa ambao tumewalaza lakini kwa mujibu wa dalili walizokuwa nazo na
vipimo vilivyofanyika hawana hali ya kuwa na ugonjwa wa Ebola,”
“Kwenye hali kama hii ambapo tunakuwa na hali kubwa ya kuweza kuhakikisha mtu ambaye anaweza akawa na dalili za ugonjwa, lazima tuweze kumuona na kumpima ili tujihakikishie kuwa hana tatizo. Lakini kiukweli sasa hatuna mgonjwa mwenye tatizo la ugonjwa wa Ebola. Tulikuwa tuna wagonjwa wawili mmoja ni binti ambaye ametokea Benin na alivyofika kwenye hospitalI ya mtu binafsi na dalili za kuwa na homa kali na viungo na maumivu kama hayo lakini baada ya kumchuKUa mgonjwa na kufanya vipimo zaidi ikajulikana ni mgonjwa mwenye matatizo ya malaria tu na kwamba hana tatizo la ugonjwa wa Ebola,” 
amesema Dk. Seif na kuongeza:

“Huyo mgonjwa tumemuondoa hana tatizo hilo. Na mgonjwa mwingine ni mgonjwa ambaye ana tatizo lingine kabisa ambalo linakuwa linapelekea kutoka damu, kwahiyo nafiriki katika kitendo hicho cha kuonekana anatoka damu kikahusishwa na hilo. Lakini kwa ujumla wagonjwa wote wawili hawamo katika tasfiri ya ujumla za dalili zile za ugonjwa na namna ambavyo tunaweza kuweka katika kundi la magonjwa haya ya Ebola huyu ni Mtanzania.”
Pia alitweet:

Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Shaaban Mwinjake (kushoto), akikanusha kuwepo kwa ugonjwa huo kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari.Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Dharura na Maafa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Elias Kwesi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Dharura na Maafa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Elias Kwesi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wakikanusha kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola nchini. 
Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Suleiman Said Suleiman akizungumza namna TAA ilivyojipanga kuhakikisha hakuna msafiri kupitia viwanja vya ndege mwenye ugonjwa huo atakayeingia nchini bila ya kugundulika.
Msaidizi wa Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Asha Omar akielezea namna Uhamiaji walivyojipanga kuhakikisha inawatambua wageni wanaoingia nchini hasa wale wanaotoka nchi zilizoathiriwa na ugonjwa huo.
Maofisa wa JNIA wakiwa kwenye mkutano huo.
Maofisa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Ofisa Afya Mfawidhi wa JNIA, George Ndaki, Mkurugenzi Msaidi wa Ufuatiliaji wa Ugonjwa, Janeth Nghambi, Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya na Ubora, Dk.Fausta Mosha na Mkurugenzi Msaidizi Afya na Usafi wa Mazingira, Elias Chinamo.
Wanahabari na wadau wengine kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Uwanja wa Ndege wakiwa kwenye mkutano huo.