Leo alfajiri niliongoza mjadala kwenye redio za Kwanza Jamii na Nuru FM kuhusiana na kongamano linaloendelea Dar la Watanzania wa Diaspora wanaokutana nyumbani, Tanzania.
Ni kwa nini tuna hofu na Watanzania wenzetu walio ughaibuni? Hofu hii ni ya kihistoria.
Kwanini kongamano hili la kwanza kufanyika lisiwe la mwisho kufanyika katika sura yake hii, kwamba maudhui ya kongamano yenyewe kuwa ni ; connect, engage, inform and ivest nako kunakosekana dhana integration kwa maana ya kujumuisha.
Hoja kubwa kwa sasa ni kwa namna gani tunawajumuisha wenzetu walio ughaibuni kupitia uraia pacha. Kwamba wakati umefika wa kubadilika na kuona kuwa uraia pacha una maanufaa makubwa kwetu kama taifa. Haipaswi kuendelea kuwachukulia wenzetu walio diaspora kama ' Ng'ombe wa Maziwa'- Fuatilia mjadala huu... kwa kubofya hapa (mjengwablog.com)