Mahojiano na mtaalamu wa uchumaji asumin: Bustani ya mapenzi yenye mauwa madogo yenye harufu nzuri, huwekwa kitandani ili bwana asitoke...

Mtaalamu wa uchumaji asumin Alwatan Kijakazi Hassan Mustafa akiwa katika harakati za uchumaji wa mauwa ya yenye harufu nzuri asumin
Blog ya Swahilivilla siku ya Jumamosi, Julai 19 2014 ilifafanya mahojiano na mtaalamu wa uchumaji wa mauwa ya asumin, Alwatan Kijakazi Hassan Mustafa, a.k.a (Kijakazi) ambaye alielezeaa mengi kuhusu umuhimu wa asumin pamoja na utunzani wake.

Katika mahojiano haya na mtaalamu wa utunzaji wa miasumini, Kijakazi Hassan Mustafa, mkaazi wa Mwembetanga Zanzibar anatuelezea mambo mbalimbali kuhusu umuhimu wa mauwa ya asumin yakiwemo kusingwa kwenye sherehe za harusi na hata kutengezea uturi pamoja na vikuba vyenye
harufu nzuri ya kunukia.

Asumin ni bustani ya mapenzi yenye mauwa madogo yenye kutoa harufu nzuri, huchumwa kwa kuwekewa kitandani ili bwana asitoke ndani wakati mwafaka wa jioni.

Ungana nasi taratibu kusikiliza mahojiano haya kwenye pleya iliyopachikwa hapa chini...Kwa mawazo zaidi wasiliana nasi kwa njia ya email: [email protected]