Mansour Himid afikishwa mahakamaniJeshi la Polisi kisiwani Zanzibar, hatimaye limemfikisha mahkamani Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano ambaye pia aliwahi kuwa Mwakilishi wa Kiembe Samaki na Waziri katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mansour Yusuf Himid.

Mhe. Mansour alisimamishwa katika Mahkama ya mkoa ya Vuga na kusomewa mashtaka ya makosa matatu ikiwemo kumiliki silaha, risasi za moto na kumiliki marisau mengi ambapo aliyakana makosa yote.

Kwa kuwa mahkama hiyo ya mkoa haina uwezo wa kutoa dhamana kwa kosa la aina ya kwanza
isipokuwa makosa mengine mawili, mshtakiwa hakupata dhamana na kesi yake iliahirishwa hadi tarehe 18 mwezi huu atakapopelekwa tena mahkamani.

Kwa mujibu wa wanasheria wake, sasa wanajiandaa kuomba dhamana kupitia Mahkama Kuu kabla ya kusomwa tena kwa kesi yake hapo tarehe 18.

Wanasheria hao wakiongozwa na wakili mzalendo Omar Said Shaaban akishirikiana na wakili Gasper Nyika ambaye ni mshirika wa wakili Fatma Karume; leo asubuhi waliwasilisha ombi mahkama kuu la “Habeas Corpus” kuhusiana na mteja wao Mhe. Mansour Yusuf Himid na lilisikilzwa na Jaji Abraham Mwampashe, ambapo aliamuru mshtakiwa apelekwe mahkamani. Baadae “court order” ilichapwa na kupelekwa polisi kwa utekelezaji.

via Zanzibar Yetu blog


Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano ambaye pia aliwahi kuwa mwakilishi wa Kiembe Samaki na Waziri katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mansour Yusuf Himid
Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano ambaye pia aliwahi kuwa Mwakilishi wa Kiembe Samaki na Waziri katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mansour Yusuf Himid