Maoni ya 'Jzellah' kuhusu wito wa Rais Kikwete kwa Diaspora

Maoni ya Jzellah aliyoyaacha hapa:

Yes, President amesema kitu mihimu sana hata alikpokuwa hapa Poland aliongea sana jambo hili la uraia pacha kuwa halipo sana kwnmye Rasimu ya katiba. Kitu ninachotaka kusema hapa ni kwamba President anaangalia upane mmoja, hatoi nafasi ya Diapora kulitetea suala hili kwenye vyombo vya habari ambalo ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu Tanzania . President anasema tuwe tunalijadili mara kwa mara katika vyombo vya habari wakati anajua kuwa sisi hatuna upenyo au milango ya kuingiza hoja zetu kwenye magazeti na radios zilizopo Tanzania.

Yeye kama President wa watanzania wote waishio nje na ndani ya nchi ana jukumu la kutupatia nafasi hiyo kwenye vyombo vya habari vya taifa au ana wajibu wa kuvitaka vyombo vya habari viwe vina toa fursa ya kujadili suala hili hadharani kama ilivyo hapa EU. Lugha aliyoitumia hapa haitupatii nafasi kwenye magazeti na TV na Radio za TZ kwani initiative inatakiwa itoke kule na hasa sana toka Ikulu. Ilitakiwa aseme " niavitaka vyombo vyote vya habari nchini hasa vya taifa viweke mjadala wa wazi juu ya suala hili la
uraia pacha.

Kwa mfano wenzetu wapolo huwa wanaweka kwenye TV ya taifa Polonia au TVP2 na radio 1 mjadala wa hadhara kuhusu kuwasaidia Diaspora wao walioko nje ya Poland, na hivyo hivyo wanafanya wajerumani n.k. Inatakiwa President kuzitaka media za serikali kuweka special open program yenye debate juu ya suala hili. Katika mjadala huo inatakiwa wawe wanakaribishwa Watanzania/ Diapora ye yote toka nchi za nje mwenye uwezo wa kuja Tanzania na kushiriki mchakato huo.

Diapsora wana pesa ya kuja TZ na kushiriki mjadala huo. Angependekeza kuwa ni lazima mjadala uwe live ili kusiwepo na kuchakachua maongezi hayo. Kuna Diaspora wengi sana nje nikiwemu mimi mwenyewe ambao kwa gharama zetu tuko tayari kuja TZ na kusimama mbele ya watanzania ili kutetea hoja yetu. Mimi ni mkereketwa wa CCM lakini nina haja ya kuwatetea Diapora wenzangu wenye nia hiyo. Kwa kifupi uraia pacha una manufaa sana kwa Watanzania na serikali yetu kwa ujumla hasa katika masuala haya ya transfer of technology toka nchi zilizoendelea.

Mtanzania ye yote ana haki ya kuondoka na kurudi nchini kwetu wakati wowote ilimradi asivunje sheria na anayo haki ya kuongeza uraia wa nchi yoyote ilimradi asiuache uraia wa Tanzania.
Nashauri Sentensi kama hii au inayolingana inatakiwa iwe kwenye Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania.
Wachina wameendelea haraka kwa kutumai system hiyo hiyo ila hawasemi wazi wamepataje technology ya USA, GERMANY, UK, JAPAN etc.

Kila siku tunapeleka viongozi wetu China kuomba msaada kutaka utajiri ambao wenzetu wameufanyia kazi kwa mbinu kama hii ya kuwatuma vijana nje kusoma na kufanya mbinu ya dual citizenship ili wasiwe na tatizo la kusafirisha technology. Leo yuko UK kesho yuko China i Vise versa. Akiwa UK anafanya kama mwingereza, akirudi China anafanya kama Mchina etc.

Ningependa Pesident awe mstari wa mbele kuelewa mbinu hii na kusaidia kumaliza suala hili.

Sisi watanzania wajinga kabisa hatutaki kuiga wenzetu jinsi wanavyofanya ili wapate technology mpya. Tanzania ina rasilmali kubwa na ya mabiloni ya USD dolars lakini utakuta sis ndo maskini kuliko nchi ambazo hazina hata chembe ya dhahabu na Almas....Kisa - tunanyanyasana wenyewe kwa wenyewe. Kipimdi cha Cold War kulikuwa na sababu za kuwanyima watanzania wasisafiri sana, lakini hakuna tena Cold war.

Siku ya Diapora pale DSM tutaongelea zaidi juu ya mjadala huu wa uraia pacha kwa manufaa ya pande zote mbili. Ahsante kunisikiliza. Jzellah, Poland