
Ndugu zangu, katika makala iliyopita namba moja, tuliangalia kwa mapana nafasi ya malengo na ndoto katika kukufikisha unapotaka katika Nyanja zote za kimaisha. Wiki hii mimi na rafiki zangu amabo kwa pamoja tunaunda kikundi cha WAKULIMA WA KISASA-TANZANIA, tulibahatika kutembelea maonyesho ya sikukuu ya wakulima mkoani Morogoro, tuliyojifunza na kuyaona yanahitaji makala nzima, wiki ijayo nitaandika jinsi umoja wetu ulivyo anza na tunafanya nini.
Leo katika sehemu ya pili nay a mwisho ya makala hii, tutaendelea kuangalia nafasi ya malengo na ndoto, mifano kadhaa ya watu waliotumia ndoto na malengo yao itatolewa na kufafanuliwa kwa kifupi sana.
Kama tunavyojua na kufahamu ( Labda kama hufahamu) hakuna binadamu chini ya jua tangu enzi za kati za mawe, aliye wahi kufanikiwa zaidi ya anavyo waza. Ukiwaza kwamba maisha ni magumu, maisha magumu yatakuandama, hii ni kanuni na inafanya kazi kabisa (The Law of Attraction). Ukiwaza juu ya uzuri wa dunia, juu ya uzuri wa ubara lako, juu ya uzuri wan nchi ya Tanzania na fursa zake, muda wote utaziona fursa zikikuijia na wewe. Katika bidhaa rahisi sana duniani ni bidhaa ya kufikiri maana haina gharama yoyote. Ni juu yako wewe kuwaza upande gani wa maisha, upande wa ubaya ama uzuri.
Una ndoto na unajiamini vya kutosha kwamba utatimiza ndoto yako lakini unajua namna ua kuifikia njozi yako? Uwezo wako wa kutunga malengo na kutengeneza mikakati ya kufikia malengo hayo ndiyo stadi muhimu unayoihitaji ili kufanikiwa. Panga vizuri mambo yako kwani bila mipango matokeo yenye uhakika ni kutofanikiwa.
Juzi tu, nilikuwa ninasikiliza mahubiri ya Mwalimu maarufu Tanzania na duniani, mwalimu Christopher Mwakasege, kwenye mahubiri yake alisema, “haijalishi unatokea mkoa gani wenye vitega uchumi vya kutosha. kinachojalisha ni jinsi gani unatumia fursa hizo....kujisifia mkoa wangu unavitega uchumi vingi wakati havichangii lolote kwenye maisha yako haina maana. Mfano Mafuta Nigeria na Norway yaligunduliwa mwaka sawa hebu angalia leo Norway iko wapi,Tanzania wakati inapata uhuru uchumi wake ulikuwa sawa na Malasyia na Korea kusini angalia leo Tanzania na hizo nchi”.
Mjasiriamali mwingine wa kimarekani kwenye kitabu chake cha Advanced Selling strategiese Brian Tracy anasema kwamba, ukimchunguza kila mjasiriamali na mtu yeyote mwenye mafanikio na aliyefanikiwa utagundua kuwa ni mchapa kazi. Hakuna mtu anayefanikwa kwa kukaa kimya na kuangalia mambo ya binadamu wenzake yanavyokwenda. Brian Tracy anasema tunafanya kazi saa 8 kila siku kwa ajili ya kuishi, lakini ukitaka mafanikio lazima uwe tayari kufanya kazi zaidi ya saa 8 kwa siku.
Lazima uwe tayari kuachana na vikao vya jioni vya unywaji kahawa, pombe na kununuliana soda au kucheza bao au kupiga soga kurushiana maneno mabaya na kuonyeshana ufundi wa kuchambua soka la ulaya wakati malengo yako yanadoda. Unapokuwa katika hatua za mwanzoni itabidi upumue, ule na unywe ndoto zako na malengo yako.
Nina dada yangu huku Iringa, huyu dada alianza kufuga na kulima kilimo cha umwagiliaji miaka miwili iliyopita, nimekuwa nikimtembelea sana, nilipo fanya mahojiano nae kuhusu kasi yake ya maendeleo na siri ya kufanikiwa aliniambia analala masaa matano tu kwa usiku mzima, na muda mwingi anautumia katika kupanga na kutekeleza malengo yangu, kilichonishangaza zaidi ni mradi wake wa sasa hivi wa ufugaji wa samaki, anasema baada ya muda atakuwa na uwezo wa kupata tani nne za samaki kila baada ya miezi minne.
Na ukitaka ndoto zako zifanikiwe, utatikiwa kuisoma dunia yako na mazingira yako. Utawasoma watu wanao kuzunguka, kwenye ujasiriamali biashara unapimwa kutokana na watu unaoshirikiana nao, kutoka kwenye kikosi chako cha menejimenti, bodi ya wakurugenzi, na wabia wenzako. Wakati wote biashara inahitaji wasidizi, hata katika biashara ndogo. Inawezekana mama mmoja uliyekutana naye kwenye basi akakusaidia kupata mkopo mahali Fulani, au bwana mmoja uliyekutana naye Kanisani au Msikitini, akakupa ushauri wa jinsi ya kuendesha biashara zako.
Ni muhimu kujenga mahusiano na watu kwani wanaweza kukusaidia kwa nanma moja au nyingine na ambao pia wewe unaweza kuwasaidia. Ili kufanikiwa katika shughuli yoyote ile unahitaji pamoja na mambo mengine kuwa na kipaji kikubwa cha kuishi vizuri na watu, na unatakiwa kuwa macho wakati wote kunasa fursa zozote zitakazotokea ili kuongeza mahusiano yako na watu.
Lakini mahusiano mema na watu yanajengwa sana na mwenendo mzuri wa uadilifu. Kwa mfano, usimuuzie mtu kitu hali a kuwa unajua hakifai kwa matumizi yaliyokusudiwa, wala usimuuzie mfanyabiashara mwenzako bidhaa kwa bei kubwa sana. Utafiti kiasi cha kumfanya ashindwe kupata faida atakapokwenda kukiuza. Kwa kufanya hivyo, huwezi kudumu katika biashara kwa muda mrefu, kwa sababu mteja wako asiporidhika na huduma yako hawezi kurudi tena kwako. Kumbuka wakati wote kwamba kila mtu utakayekutana naye katika harakati zako za kutafuta riziki, basi ujue nayeye pia anatafuta riziki.
Nimesoma makala iliyo nishitua na kunifumbua macho zaidi makala hii yenye kichwa cha “Is Your Brain Limiting Your Entrepreneurial Success” (unaweza kuisoma mkala hii ukiitafuta kwenye tovuti ya google) makala iliyoandikwa na mwanadada mjasiriamali Meiko Patton, Meiko anasema ubongo wetu ni sawa na kiwanda kikubwa sana ambacho kinauwezo wa ajabu, anasema huhitaji kuwa na digrii ya falsafa wa ya uzamili ya Biashara, ama uwe fundi na mwanasayansi wa roketi za kijeshi, ili uweze kufanikiwa katika mambo yako ya ujasiriamali.
Wapo wajasiriamali wengi tu waliofanikiwa hapa Tanzania na kwingineko duniani kwa kiasi kikubwa sana lakini hawakumaliza hata masomo ya sekondari. Hata hivyo, wajasiriamali hawa wamefanikiwa kufikia hatua hii ya juu kabisa katika mafanikio kwa kupata fedha na kutimiza malengo yao mengine kwa sababu walikuwa tayari kujifunza, kupanga na kuishi maisha ya ndoto zao. Moja ya malengo yangu makubwa ni kugusa maisha ya jamii, nimekuwa nikitumia muda wangu mwingi kuwashirikisha watu juu ya kilimo na hasa kilimo cha miti maana ndio ndoto yangu kubwa na ninayoiishi.
Kuna wale ambao walilishwa sumu wakiwa masomoni, kwamba kusoma ni mitihani, wakisikia ama wakimuona mtu anasoma labda ndani ya basi basi akili na mawazo yao yanaelekea kwenye mitihani . Kuwa tayari kujifunza si lazima kurudi darasani. Ili ufanikiwe lazima uwe tayari kuuliza maswali, kudodosa kupenda na kuwa tayari kupokea maarifa mapya. Hali ya kuwa tayari kujifunza inakuwa muhimu sana, hasa ukizingatia ulimwengu wetu huu wa sasa unaokabiliwa na mabadiliko makubwa na yanayotokea harakaharaka sana kutokana na Utandawazi.
Hakuna mtu aliyesema kwamba njia ya kufanikiwa ni rahisi. Licha ya dhamira na ari yako kubwa, na uchapaji kazi wako wa hali ya juu. Lakini bado unaweza usifanikiwe.
Katika makala yake nyingine mwanadada Meiko Patton katika “Successful Entrepreneurs Do These 5 Things Daily” amaeelezea kwamba, Baadhi ya wajasiriamali waliofanikiwa walikutana na misukosuko mingi na baadhi yao kufilisika, lakini walifanikiwa kusimama tena haraka na kupata mafanikio makubwa baadaye.
Ujasiri wako wa kuendelea kuvumilia wakati wa matatizo na uwezo wako wa kurudi tena baada ya maudhi ya muda mfupi vitakuhakikishia mafanikio. Lazima ujifunze namna ya kunyanyuka tena baada ya kuanguka. Ustahimilivu na ung’ang’anizi wako ndiyo kipimo kinachoonyesha kwa kiasi gani unajiamini. Kumbuka, ukistahimili hakuna kitakachokuzuia kufanikiwa.
Thomas Huxley aliwahi kusema, Nidhamu ni kufanya kila unachopaswa kufanya, wakati ule unaopaswa kufanya, iwe unapenda kufanya hivyo au la. Nidhamu binafsi ni ufunguo wa mafanikio. Uwezo wa kujilazimisha kufanya mambo ndiyo siri ya mafanikio- kufanya mambo ambayo wengine hawapendi kuyafanya, kwenda umbali moja zaidi wakati wengine wamechoka, hawako tayari kuendelea, ndiyo nidhamu binafsi itakayokusaidia kufanikiwa.
Kwakumalizia makala hii, Ninamfahamu Joshua Steimle, katika kitabu chake cha “How To Win When You Fail” anasema yaelekea maisha yetu ya leo yanahitaji nidhamu zaidi kuliko ya vizazi vilivyotangulia ingawa yana uhuru zaidi. Akifafanua zaidi anasema saa zetu za kazi zinaelekea kukabiliwa na majukumu mengi ya kufanya, ingawa bado tuna hiyari nyingi zaidi za kuchagua.
Binadamu wote wenye mafanikio duniani hawachoki kutafuta..!