Mgombea Urais wa Brazil afariki katika ajali ya ndege

Mgombea Urais wa Brazil kwa tiketi ya Brazilian Socialist Party, Eduardo Campos, 49, ambaye Kitaaluma ni Mchumi,  ameaga dunia leo katika ajali ya ndege iliyotokea huko pwani kusini mwashariki mwa jiji la São Paulo.

Chombo cha habari cha nchini humo, O Globo kimesema kuwa Campos alikuwa abiria katika ndege ya kukodi ya Cessna ambayo ilianguka katika mji wa Santos asububi ya Jumatano ya leo ikiwa jumla ya watu saba, akiwamo mke na mtoto wa marehemu. 

Taarifa zinasema hali mbaya ya hewa huenda ikawa ndiyo chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo iliyokuwa ikijiandaa kutua.