Mjumbe wa Bunge la Katiba adai kupigwa na vijana wa CHADEMA

Mh. Edward Lowassa akimjulia hali Mgoli hospitalini, wote wako kamati namba 12. (picha: Fikra Pevu)

Mjumbe wa bunge maalum la katiba kutoka kundi la 201,Thomas Magnus Mgoli amelazwa katika hospital ya mkoa Dodoma baada ya kudai kupigwa na wanaodaiwa kuwa 'vijana ambao mashabiki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)'.

Kwa mujibu wa FikraPevu akiwa kitandani hospitalini, Mgoli amesema alishambuliwa na vijana hao jana usiku majira ya saa moja eneo la area D anakoishi.

Amedai kuwa hukutana na vijana hao mara kwa mara anapokwenda dukani na huzungumzia masuala ya bunge hilo, lakini hiyo jana walimshambulia kwa kumuambia kuwa yeye ni CCM.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta akimjulia hali mjumbe wa Bunge Maalum kutoka kundi la 201 Mhe. Thomas Mgoli aliyelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kujeruhiwa na watu wasiojikana wakati akipata huduma katika duka moja lililopo karibu na mahali anapoishi Mjini Dodoma. (picha: Owen Mwandumbya)