Mkutano Mkuu wa CCM Uingereza, Agosti 2014


MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI UINGEREZA

30th AUGUST 2014.

HAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA UINGEREZA LINAPENDA KUWATANGAZIA WANACHAMA NA WAPENZI WOTE WA CCM KUTOKA PANDE ZOTE ZA UINGEREZA KWAMBA KUTAKUWA NA MKUTANO MKUU WA TAWI TAREHE 30.08.2014 UTAKAOFANYIKA KATIKA JIJI LA READING KATIKA ANUANI IFUATAYO;
THE PAVILION (FORMERLY RILEYS CLUB)
143 – 145 OXFORD ROAD READING
RG1 7UP

KATIKA MKUTANO HUO PIA KUTAFANYIKA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA TAWI LA CCM UINGEREZA ILI KUJAZA NAFASI INAYOACHWA WAZI NA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA TAWI HILI TOKA KUANZISHWA KWAKE NDUGU AINA OWINO ANAYENG’ATUKA NAFASI HIYO.

WAGOMBEA WA NAFASI YA MWENYEKITI WA TAWI WALIOPITISHWA NA HALMASHAURI KUU YA TAWI ILIYOKUTANA TAREHE 02.08.2014 NI;

PETER GABAGAMBI

KANGOMA KAPINGA 

SAID SURURU

WANACHAMA WOTE NA WAPENZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI UINGEREZA MNAHIMIZWA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA MKUTANO HUO ILI KUTUMIA NAFASI YAKO PEKEE KUMCHAGUA KIONGOZI ATAKAYELETA MABADILIKO KATIKA TAWI.

Imetolewa na Idara ya Itikadi Siasa na Uenezi 
Chama Cha Mapinduzi Tawi La Uingereza.