Moto unaunguza Msikiti wa Mtambani, Kinondoni, Dar

Picha ya jengo la Msikiti wa Mtambani ulioko katika maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam iliyopigwa wakati moto unaliunguza jengo hilo. Taarifa za chanzo cha moto huo, madhara na hasara yake havijafahamika
Imeelezwa na wananchi kuwa moto huo ulianzia kwenye madrasa ambayo ni sehemu ya juu ya jengo hilo kabla ya kushuka katika vyumba vya chini.

Vyumba vya Shule ya Sekondari ya Kiislam ya Mivumoni (Mivumoni Islamic Seminary) iliyopo ndani ya Msikiti huo vimeungua.

Eneo hilo ambalo lilikuwa likitumika kama mabweni ya Wanafunzi wa Shule hiyo, maabara na Ofisi za
Walimu limeteketea kabisa, hakuna kilichookolewa.

Othman Michuzi aliyekwenda kwenye eneo hilo amesema chanzo cha moto huo inadaiwa ni hitilafu ya umeme iliyokuwepo kwenye bweni la Wasichana Wanafunzi wa Shule hiyo.

Hakuna mtu yeyote aliepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo.

Picha zifuatazo ni kutoka kwa Othman Michuzi na Francis Dande...

 Moto ukiunguza jengo la Msikiti waMtambani
 Wananchi wakichota maji katika harakati za kusaidia kuzima moto.
 Askari wakiimarisha ulinzi.
 Mfanyakazi wa kampuni ya Altimate akiongeza maji kwenye kwa kutumia ndoo baada ya gari lao kuishiwa maji.
 Gari la zimamoto likiwa limezungukwa na vijana waliokuwa wakisaidia zoezi la kuzima moto katika msikiti wa Mtambani Kinondoni.
 Baadhi  ya vijana wakisaidiana na wafanyakazi wa Kikosi cha Zimamoto kutoka kampuni ya Altimate Security kuweka maji katika gari baada ya gari hilo kuishiwa maji.
 Moto ukishika kasi.
 Moto ukienea katika eneo la juu.