Kila uchao lazima kuna mahali mtu atakumbushia watu kuhusu kunawa mikono.
Siku nenda, rudi zimekuwepo kampeni za kuhamasisha unawaji mikono hata katika maeneo ambayo upatikanaji wa maji ni shida, kwa kuwa hata hayo kidogo, bila msingi wa afya njema wa kunawa mikono, hayatakuwa na faida yoyote ikiwa matumizi yake hayatafanywa kwa mikono iliyo safi.
Baada ya kufumuka kwa ugonjwa wa Ebola, sasa ndipo watu wanapotilia maanani na kuona umuhimu wa kunawa mikono bila shuruti, aibu wala kukumbushwa.
Nchini Liberia ambako ni mojawapo ya nchi zilizokumbwa na ugonjwa wa Ebola, watu wamepatwa na kiwewe cha kunawa mikono kama mtu mwenye dirty vs clean hands OCD (Obsessive Compulsive Disorder).
Maji yanapatikana wapi? Mbele ya hofu ya kifo, yatapatikana tu! Hata kutoka mawinguni...
...A police officer is shouting at a woman, "You have to wash your hands." She says, "I agree but how can I wash my hands without water?" This is the rainy season, people are looking up at the sky. Another downpour is coming. A guy on motorcycle says, "Would it be okay if we wash our hands in the rain?"
Do you get any stares for wearing surgical gloves?
No one bats an eye. As we were landing in Liberia Sunday morning on a flight from Casablanca, the flight attendants put on surgical gloves and a few other passengers did.