TAMASHA la Usiku wa Matumaini, Dar (Dar Night of Hope 2014) lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar lilikuwa ni full msisimko kutokana na matukio mbalimbali yaliyofanyika.
Staa kutoka nchini Nigeria, Yemi Alade akipiga shoo usiku huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Yemi Alade akipiga shoo usiku huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
BONGO MOVIES VS BONGO FLEVA
Wakati mechi hiyo ilipokuwa ikikaribia kuanza, umati ulilipuka kwa shangwe baada ya kumuona Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba alipokuwa alipoonekana akipasha misuli na wenzake.
Wengi walikuwa wakishangilia wakidai ni siku nyingi hawajamuoana uwanjani, huku wengine wakishangilia kwa kuimba wimbo wake mpya wa Mwana.
Kama hiyo haitoshi haitoshi, shangwe zaidi liliongezeka baada ya Kiba kufunga bao ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo na kuwafanya Bongo Fleva waibuke kidedea kwa mara nyingine hivi kumfanya kuwa nyota kwenye tamasha hilo.
BONGO MOVIES WACHEZA KIDUKU
Licha ya kufungwa, mashabiki wa Bongo Movies ndiyo walionesha kushangilia zaidi ya mashabiki wa Bongo Fleva ambao ndiyo walikuwa washindi.
Walicheza staili ya kiduku ile mbaya huku wakishangiliwa na umati uliofurika uwanjani hapo.
WABUNGE SIMBA VS YANGA
Wakati wa mechi ya wabunge, vituko ndiyo ilikuwa balaa. Kuna wakati baadhi ya waheshimiwa wabunge walikuwa wamechoka kiasi cha kushindwa kusogea lakini mwisho wa siku ilikuwa ni burudani kwani waliweza kubadilishana, wengine wakachukua nafasi. Hadi mtanange unamalizika, wabunge wa Yanga waliibuka kidededea kwa ushindi wa mabao 3 kwa 2.
Matukio mengine yaliyosisimua siku hiyo ni kama wasanii wa Bongo Fleva, Juma Nature, Shilole na wengineo ambao walipanda stejini kwa nyakati tofauti na kutoa burudani baab’kubwa.
Tamasha la Usiku wa Matumaini mwaka huu lilikuwa noma sana!
Makamu wa Rais wa Tanzania, Mohamed Ghalib Bilal amelipongeza wazo la Tamasha la Usiku wa
Matumaini lililoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers, jana kuwa ni zuri.
Alimpongeza Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo kwa kuandaa tamasha hilo kwani linaunganisha Watanzania wote.