Mtanzania aliyekwenda Mkutanoni aomba hifadhi AustraliaWaafrika wapatao 25 wameripotiwa na vituo vya habari vya nchini Australia kuwa wameomba hifadhi nchini humo punde tu ulipomalizika mkutano wa 20 wa Kimataifa uliozungumzia masuala ya VVU/UKIMWI mwezi uliopita.

Inaripotiwa kuwa mara baada ya mkutano kuisha tarehe 25 Julai, wajumbe hao waligoma kuondoka nchini humo na sasa wapo katika wakati mgumu wa malazi, mavazi na chakula.

Mmoja wao ambaye anatokea Tanzania lakini aligoma kutaja jina lake kwa sababu za kiusalama amekiambia kituo cha habari cha ABC kuwa akiwa nchini Tanzania, hujishughulisha na watu wanaoishi na VVU na albino na hivyo kuhatarisha maisha yake.

Amesema kwa mfano mwezi Machi mwaka huu almanusura apoteze maisha yake baada ya kukimbizwa na watu kadhaa alipokuwa akitoka kutizama mechi ya soka. 
"Those people they saw me and then they started chasing me, it was around 8pm in the evening...."
amekaririwa kusema na kuongeza:
"So I got a very bad accident ... almost like dying. They wanted to kill me. After that crash, they disappeared completely because so many people came to give me help"

"I don't have faith [in] my own state government to protect me against these people"

"I learn that Australia has a human rights reputation, that's why I seek protection here"
Amesema anatarajia kuwasilisha fomu za kuomba hifadhi baadaye mwezi huu.

Unaweza kusoma zaidi habari hii kwenye:
African delegates from Melbourne AIDS conference seeking asylum in Australia
au