NAFASI ZA MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA MASHINE ZA KUTOTORESHA VIFARANGA VYA KUKU.
Taasisi ya RafikiElimu Foundation kupitia MRADI WA ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINJI inatangaza nafasi za MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA MASHINE ZA KUTOTOLEA VIFARANGA WA KUKU.
Mashine zitakazo fundishwa kutengeneza ni INCUBATOR (MANUAL & AUTOMATIC) zenye uwezo wa kutunza joto kwa sasa 48 pamoja na kutotolesha mayai kuanzia 240 hadi 5000.
Vile vile yatatolewa mafunzo ya UTENGENEZAJI WA MAJIKO SANIFU NA NISHATI MBADALA.
ADA YA MAFUNZO :
Ada ya mafunzo haya ni SHILINGI ELFU ISHIRINI NA TANO TU. (Tshs. 25,000/=)
TAREHE YA KUANZA KWA MAFUNZO
Mafunzo haya yatafanyika kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 01 SEPTEMBA 2014 hadi tarehe 05 SEPTEMBA 2014
FOMU ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO :
Fomu za kujiunga na mafunzo haya zinapatikana ofisini kwetu kwa gharama ya SHILINGI ELFU KUMI NA TANO TU ( Tshs.15,000/=).
MWISHO WA KUCHUKUA FOMU :
Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 28 AGOSTI 2014.
Ofisi zetu zinapatikana katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU.
JINSI YA KUFIKA OFISINI KWETU:
Kufika ofisini kwetu, panda daladala za UBUNGO- CHANGANYIKENI kisha shuka kituo cha TAKWIMU halafu tembea hatua ishirini mbele kisha tazama upande wako wa kulia utaona ofisi imeandikwa RAEFO TANZANIA.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu 0784406508.
Kwa taarifa zaidi kuhusu mafunzo ya utengenezaji wa mashine za kutotolea vifaranga, tembelea: www.rafikielimu.blogspot.com