Nchemba amsimika Asas kuwa Kamanda wa UVCCM Iringa; Naye asimikwa kuwa Chifu wa Wahehe

Mwigulu Nchemba katika vazi la kichifu baada ya kutawazwa kuwa Chifu wa Wahehe alipofika kumtawaza Salim Asas kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Iringa.


Baada ya kuingia Iringa Mjini, Nchemba akaamua kuingia mtaani kutembelea matawi ya Chama Cha Mapinduzi na kuzungumza na Wananchi. Hapa msafara wake ukiwa soko la mitumba Iringa Mjini.

Vijana wa CCM Iringa Mjini wakiwa mitaani Iringa Mjini.


Chipukizi wa Chama Cha Mapindizi Iringa Mjini wakiwa tayari kwa kumpokea Mgeni Rasmi Mhe. Mwigulu Nchemba.

Mwigulu akipewa mapokezi na chipukizi wa Chama cha Mapinduzi Iringa Mjini.


Msafara wa Naibu Katibu Mkuu CCM Bara ukielekea kwnye viwanja vya mkutano.

Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mwigulu Nchemba akiingia viwanja vya Mwembetogwa Iringa Mjini tayari kwa kumsimika Kamanda wa UVCCM Ndugu Salim Asas.
Vijana wa Chama cha Mapinduzi Iringa wakifikisha ujumbe wao kwa Watanzania.

Kiongozi wa madereva wa bodaboda na bajaji Iringa Mjini akisalimiana na Mhe. Nchemba.

Naibu Katibu Mkuu CCM Bara akielekea kupanda jukwaani tayari kwa kuzungumza na wakazi wa Iringa Mjini.

Comrade Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi.

Nchemba akisisitiza umoja ndani ya Chama na Jumuiya zake.


Sehemu ya mamia ya Wananchi waliofurika uwanja wa Mwembetogwa kushuhudia zoezi la kuapishwa kwa Kamanda wa UVCCM Ndugu Salim Asas.

Mwigulu Nchemba akzungumza na Wananchi waliofurika uwanja wa Mwembetogwa namna Wizara yake ilivyoanza mikakati ya kuhakikisha kuwa fedha za Watanzania zinatumika ipasavyo kwenye kazi za maendeleo. Pia lisisitiza kubana matumizi serikalini ndiyo kipaumbele cha ofisi yake kwa wakati wote wa utendaji kazi wake.

Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Comrade Mwigulu Nchemba akipata picha ya pamoja na Kamanda wa UVCCM Iringa Ndugu Salim Asas. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Bi. Jesca Msambatavangu.


Mhe. Nchemba akiwaaga Wananchi waliofika kwenye shughuli ya kusimikwa kwa Kamanda wa UVCCM Iringa.

Picha/Maelezo: Festo Sanga.