Nchemba asitisha safari kwa muda ili kuhudumia majeruhi

Nchemba akiendelea kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi kabla ya kumkimbiza kwenda hospitali ya Wilaya ya Mikumi.

Na Festo Sanga.

Naibu Waziri wa Fedha na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mheshimiwa Mwigulu Nchemba jana alisitisha safari yake kwa muda wakati akielekea Iringa, na kuwasaidia majeruhi wa ajali ya lori lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea barabara ya Iringa na kupatwa na ajali.

Ajali hiyo ambayo ilitokea mbele ya Nchemba aliyekuwa nyuma ya lori hilo kabla ya kugonga ukuta na
kuanguka, haikuleta madhara makubwa.

Mhe. Nchemba ambaye mara kadhaa amekuwa akisaidia kuokoa majeruhi kwenye ajali anapokutana nazo barabarani, hata kwenye ajali hii alilazimika kuhakikisha majeruhi wanaokolewa na kukimbizwa hospitalini. Katika ajali hiyo Mhe. Nchemba alitumia boksi lake la Huduma ya Kwanza (First Aid Kit) kuwahudumia majeruhi hao.

Wananchi na madreva waliosimama kwenye ajali hiyo walimpongea Nchemba kwa kuwasaidia Watanzania wenzake kwenye ajali hiyo na kutoa wito kwa viongozi wengine kuiga mfano huu kwani imekuwa ikitokea viongozi wanapoona ajali huwa hawasimami kwa madai kwamba wanawahi ratiba za kazi zao.
Mwigulu Nchemba akizungumza na kondakta wa gari lililopata ajali mara baada ya kumnasua kwenye roli hilo.

Mwigulu Nchemba akiangalia sehemu aliyokuwa amebanwa kondakta wakati lori hilo likianguka na baadaye kuinuka kutokana na kugonga ukuta pembezoni mwa barabara ya Iringa-Morogoro.

Nchemba akitoka huduma ya kwanza kwa majeruhi wa ajali hiyo.

Huyu ni dereva akijaribu kuwasha gari hilo.