Ndege yaanguka Iran na kuua 39 ikiacha majeruhi 9


Ndege ya abiria ya shirika la Sepahan Airlines imeanguka nchini Iran na kuua abiria wapatao 39 huku ikiacha majeruhi 9 kati ya watu wote 48 (abiria na wafanyakazi) waliokuwemo ndani.

Inasadikiwa kuwa huenda hitilafu ya injini moja katika ndege hiyo ikawa ndiyo chanzo cha ajali hiyo.

Kituo cha runinga cha IRNA kimekaririwa kikisema kuwa ndege hiyo ilianguka mapema asubuhi ya Jumapili ya leo katika makazi ya watu katika mji wa Azadi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mehrabad Magharibi yapata kilometa tano hivi kutoka mji wa jiji la Tehran ilipokuwa ikielekea Tabas.

Ndege hiyo inayojulikana kama Iran 141 ilitengezwa nchini Iran kwa teknologia ya Ukraine.

Rais wa nchi hiyo, Hassan Rouhani ameagiza kusitishwa kwa safari zote za ndege ya Iran-140 na kufanya uchunguzi.