NMB
inashiriki maonyesho ya wakulima ya nane nane katika mikoa saba huku
huduma zote za kibenki zikiwa zinafanya kazi katika mabanda yake kama
kuweka na kutoa fedha, kupata taarifa za mikopo hasa ya kilimo.
NMB
inashiriki maonyesho ya nane nane katika mikoa ifuatayo; Lindi ambako
yanafanyika kitaifa, Morogoro, Dodoma, Tabora, Mbeya,Arusha na
Kagera.
Wakulima
pia wanaotembelea mabanda ya NMB kote nchini watapata fulsa ya
kukutana na wataalam wa kilimo na pembejeo, vyama vya ushirika na
hivyo kuwa na fulsa nzuri za wao kupata taarifa sahihi na ushauri wa
jinsi ya kutumia benki kunufaisha shughuli zao za kilimo.
Kwa
kuwa moja ya malengo ya NMB ni kuhakikisha inasaidia ukuaji wa kilimo
na kukifanya kuwa cha kibiashara, yenye malengo la kumkwamua mkulima.
Hii ni fursa nzuri kwa wakulima, wafanyakazi wa serikali na
wajasiriamali kuweza kufika kwenye mabanda ya NMB ili kujionea huduma
ambazo benki inatoa.
Kilimo
ni uti wa mgongo kutokana na ukweli kwamba karibia 80% ya watanzania
wanajishughulisha na kilimo.Kwa kutambua hilo, NMB ipo karibu yao
zaidi katika kipindi hiki cha Nane Nane kwa kuleta huduma za
kuwanufaisha.
Kauli
mbiu ya ‘Kilimo na Mifungo ni biashara’ kwa mwaka huuimeifanya
NMB kushirikiana na serikali katika kufanikisha maonyesho ya nane
nane katika mikoa yote saba.
Benki
ya NMB inatoa huduma mbali mbali za kilimo ikiwa ni pamoja na akaunti
maalumu ya Kilimo yaani ‘Kilimo
Account’ ambayo
inamruhusu mkulima kuweza kujipatia mikopo mbali mbali ili kuweza
kuinua uchumi wa Nchi.