Jarida
la kimataifa la Euromoney la Uingereza limeitaja NMB kuwa benki bora
Zaidi kwa mwaka 2014 katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika
jijini London hivi karibuni. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa NMB
kutajwa kama benki bora Tanzania ambapo mwaka 2013 pia NMB iliibuka
kidedea na kutajwa benki bora Tanzania-2013.
Kila Mwaka, Jarida la Euromoney huandaa hafla ya kuyatambua Zaidi ya
Makundi 20 ya bidhaa za kitaasisi za kifedha zikiwemo benki kote
duniani kwa kuagalia benki bora na ya kiwango cha juu kwa
kila bara na
benki bora katika nchi takribani 100 duniani kote. Tuzo hii huzitambua
taasisi za kifedha duniani kote ambazo zimepata mafanikio ya hali ya juu
katika maeneo yao, kwa kuonyesha ugunduzi na kupata mafanikio ya
kifedha kila mwaka.
Jopo la wataalam kutoka mataifa mbalimbali na wenye utaalamu
mbalimbali hupitia taarifa zinazowasilishwa na taasisi zote za kifedha
duniani na kutangaza washindi.
Ndani ya miezi 12, benki ya NMB
imeanzisha huduma mbali mbali za kibenki na hivyo kuendelea kuwafikia
wateja wa huduma za kibenki kuanzia kuweka akiba, kutoa na kuchukua
fedha mijini na vijijini. Kama benki ya kitanzania yenye wateja Zaidi ya
milioni 2, Mpango wa NMB unadhihirisha dhamira yake kuhusu elimu juu ya
masuala ya kifedha kwa watanzania.” Alisema Mark Wiessing.
“Tunatoa shukrani zetu wa wateja, wafanyakazi na washika dau wote
kwa kuwa sehemu ya mafanikio haya makubwa kwa benk, “ alisema Wiessing
na kuongeza kuwa NMB itaendelea na ahadi yake ya kuwapa huduma bora
wateja wake sasa na siku za mbeleni.
Wiessing aliongeza pia kuwa tuzo hiyo inaongeza kwenye hazina ya
tuzo ambazo benki imezipata katika miezi 12 huku akizitaja baadhi kuwa
ni benki bora ya mwaka kutoka jarida la Banker, Mamlaka ya mapato
Tanzania (TRA) wakiipa NMB tuzo ya mlipakodi anaefuata sharia katika
taasisi za kifedha nchini. Mwaka 2013 jarida la Euromoney pia liliitaja
benki kuwa Benki bora Tanzania huku taasisi ya Super Brand ya Kenya
ikiitaja benki bora Tanzania katika taasisi 20 bora Tanzania kwa
2013/3014 na Jarida la the Banker pia liliitaja NMB kuwa benki bora ya
kibiashara Afrika Mashariki.