NMB Yazindua tawi la Nanyumbu

NMB katika kuongeza idadi ya matawi yake na kuhakikisha inawafikia watanzania wengi na kila kona nchini, jana imezindua tawi jipya la wilaya mpya ya Nanyumbu katika mkoa wa Mtwara.

Kwa sasa NMB imefikisha matawi Zaidi ya 150 na wateja Zaidi ya milioni 2 huku ikijivunia ATM mashine Zaidi ya 500 nchi nzima. Hiyo ni idadi kubwa kuliko benki yoyote Tanzania.

Ufunguzi wa tawi hili ni Faraja kubwa kwa wakazi wa Nanyumbu ambao wamekuwa wakipata tabu kufuata huduma za kibenki wilayani Masasi. Uwepo wa NMB pia utarahisisha biashara kwa wakazi wa Nanyumbu kwani wengi wao wanafanya biashara na wananchi wa Msumbiji. Ubadirishaji wa fedha za kigeni pia ni mojawapo ya huduma itakayosaidia wakazi wa Nanyumbu nan chi ya Msumbiji.NMB pia ili kusogeza huduma Zaidi kwa watanzania, measisi ubunifu mkubwa katika soko la Tanzania ikiwa ni pamoja na huduma za benki kwa njia ya simu yaani NMB mobile , Pesa Fasta na malipo kwa kutumia mashine za ATM. NMB inaendelea kujikita katika kutoa huduma kwa makampuni makubwa, masoko ya kifedha pamoja na huduma za kusaidia makusanyo ya kifedha na biashara. Lakini Pia  imekuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya kilimo na imeanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani kupitia vyama vya ushirika nchini.


Kaimu mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Kristofer Maga (katikati) akikata utepe kufungua tawi la NMB Nanyumbu

Meneja wa NMB kanda akitoa maelezo mafupi baada ya uzinduziMmoja wa wafanyabiashara wa Wilaya ya Nanyumbu akizungumza