Rais Kikwete amteua Balozi mpya wa Tanzania nchini Rwanda

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Ndugu Ali Idi siwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kigali, nchini Rwanda.

Uteuzihuo umefanyika kufuatia kuwepo kwa nafasi wazi iliyoachwa na Balozi Dkt Mwita Marwa Matiko ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria. Ndugu Ali Siwa amekuwa katika utumishi wa umma tangu mwaka 1977 na uweza kushikanafasi mbalimbali za uongozi.

Aidha, kati ya mwaka 2001 na sasa, Balozi Metule Ndugu Siwa alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Abu Dhabi iliyoko nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates); Moscow, nchini Urusi na baadaye Berlin, nchini Ujerumani.

----- MWISHO -----

(John M. Haule)
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NJE
NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.

26 AGOSTI, 2014..