Rais Kikwete azindua TeleMedicine; Aahidi kutafuta soko la mazao ya chakula nje ya nchi

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa  kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa  kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014

Rais Jakaya Kikwete amezindua mradi mpya wa huduma ya afya kwa njia ya mtandao (TeleMedicine) katika kituo cha afya cha Mwaya, wilayani Ulanga, mradi ambao ni moja ya utekelezaji wa sera ya afya ya mwaka 2007 wenye lengo la kuboresha huduma za afya vijijini ili kupunguza vifo vya watoto wenye umri chini ya imaka mitano na wajawazito.

Rais alisema huduma hizo zitasaidia kutatua matatizo yaliyoshindikana katika zahanati na kwamba watahakikisha huduma zote muhimu kama ya upasuaji, zitakuwepo.

Rais pia aliaidi kushughulikia tatizo la soko la mpunga katika wilaya hiyo. Alisema serikali itatafuta masoko ya mazao ya chakula nje ya nchi ili kusaidia wakulima kuuza kwa tija.
“Nitahakikisha tunatafuta soko la mazao ya chakula nje ya nchi ambapo nilikwishawaagiza mawaziri nchi ya Sudan Kusini kuyatafuta, jambo litakalowezesha wakulima kuuza kwa faida,”
Taarifa ya maanishi via gazeti la UHURU
Taaifa kwa picha ni kutoka Ikulu.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete pamoja na Wabunge Mhe Abdul Mketeme (kushoto) na Mhe Getrude Rwakatale (kulia) wakifunua pazia kwa pamoja kuashiria kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea akikagua wodi mpya ya kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa maeneo mbali mbali ya kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini baada ya kukifungua Agosti 22, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wazazi baada ya kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014