Rais Kikwete na Mama Salma watembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library) na kujionea nafasi kubwa iliyotolewa kwa Tanzania na zawadi ambazo Rais Bush alizipata katika ziara yake rasmi ya Tanzania wakati akiwa Rais wa Marekani. Maktaba hiyo ya kuvutia inaendeshwa kwa teknolojia ya kisasa kabisa ya habari na mawasiliano.
Rais Kikwete alikuwa amesimama mjini Dallas kwa muda akiwa njiani kutoka Washington D.C., kwenda Houston, jimbo hilo hilo la Texas kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara wa mafuta na gesi ambao wanataka kuwekeza katika sekta hiyo katika Tanzania.
Rais Kikwete amekuwa katika Marekani kwa ziara ya kikazi ya siku tisa, ambako miongoni mwa mambo mengine, amehudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Marekani na Afrika uliofikia kilele chake jana kwa kikao kilichoendeshwa na Rais Barack Obama wa Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington D.C.