![]() |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika na wake zao, Mama Salma Kikwete na Mama Getrude Mutharika, wakiongea kwa furaha walipokutana kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani. Rais Kikwete na Rais Mutharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili. |