Rais Kikwete sasa ni Chifu Chidukila baada ya kutawazwa na Chifu Kingalu wa Waluguru



CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumtawaza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014. Rais Kikwete pia alipewa jina la CHIDUKILA, lenye kumaanisha "muibukaji", kwa maana ya kwamba Rais Kikwete ana uhuru wa kuibuka kijijini Kinole bila taarifa wala kusubiri kualikwa.




CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumvika mgolole Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014




CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimvika mgolole Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo






CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimvipa pama lililosukwa kwa ukindu Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo




CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimkabidhi kifimbo maalumu Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo




CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimuonesha Rais Jakaya Mrisho Kikwete namna ya kuweka kifimbo maalumu begani wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo




Mke wa Chifu Kingalu akimkabidhi Mama Salma Kikwete shuka katika sherehe hizo




Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akifurahia wakati wa sherehe hizo




Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akifurahia kifimbo maalumu alichokabidhiwa wakati wa sherehe hizo




Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akiongea na wananchi wakati wa sherehe hizo




Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akihutubia wakati wa sherehe hizo




Umati wa wananchi ukimsikiliza Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila wakati wa sherehe hizo



Hotuba ikiendelea



Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akisikiliza maelezo Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Morogoro Injinia Juliana J. Msaghaa akieleza juhudi za upatikanaji wa maji safi na salama wilayani humo wakati wa sherehe hizo


Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila wakati wa sherehe hizo




Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akifurahia pama lake wakati wa sherehe hizo




CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14 akibadilishana mawazo na Rais Kikwete wakiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe Joel Bendera na kushoto ni msaidizi wa Chifu Kingalu

Mama Salma Kikwete akihutubia wananchi wakati wa sherehe hizo, akisisitiza umuhimu wa kinamama kujiunga na SACCOS pamoja na kupambana na ugonjwa wa Fistula kwa wakati muafaka



Rais Kikwete akiwaaga wananchi wa Kinole baada ya sherehe hizo.

Picha zote: Ikulu