Serikali yampiga marufuku raia wa Iraq kuingia nchini

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Idara ya Uhamiaji

Raia wa Uholanzi mwenye asili ya Iraq, Shirwan Naseh aliyezuliwa kuingia nchini na Idara ya Uhamiaji

Idara ya Uhamiaji nchini ni moja ya Taasisi za Ulinzi na UsalamA iliyo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiwa na jukumu kuu la kudhibiti na kuwezesha uingiaji, ukaazi na utokaji nchini wa raia na wageni.

Katika taarifa hii kwa vyombo vya habari, Idara inakusudia kuelezea umma kuhusu kuzuiliwa kuingia nchini kwa Bw. SHIRWAN NASEH ISMAIL, RAIA WA NETHERLAND, mwenye PASIPOTI NA. BRR40RK68 iliyotolewa tarehe 15 Julai, 2014.

Raia huyu wa Uholanzi mwenye asili ya Iraq, amekamatwa jana tarehe 21.08.2014 majira ya saa
 8.35 usiku akijaribu kuingia nchini kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki Nam. 603.

Bw. Shirwan ni miongoni mwa watu wanaoshukiwa kuhusika na mtandao wa usafirishaji wa wageni kutoka mataifa ya Syria, Iran na Iraq kwa kutumia pasipoti bandia za mataifa mbalimbali ya Ulaya.

Baada ya kuzuka kwa wimbi hilo, Idara kwa kushirkiana na vyombo vingine vya Usalama vya Kitaifa na Kimataifa ilifuatilia kwa karibu taarifa za watuhumiwa wa mtandao huo na hatimaye leo, ikamtia mbaroni Bw. SHIRWAN NASEH ISMAIL.