Taarifa ya Kamanda Kova kuhusu kukamatwa kwa askari bandia

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI

JESHI LA POLISI TANZANIA


PRESS RELEASE
04/08/2014

ASKARI POLISI FEKI WA USALAMA BARABARANI ALIYEKUWA ANATAPELI WANANCHI AKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM


Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam linamshikilia na kumhoji mtu mmoja aitwaye ROBSON S/O SEIF MWAKYUSA EMMANUEL, miaka 30, Mkazi wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kujifanya afisa wa Polisi kikosi cha Usalama barabarani akiendelea na kazi za ukaguzi wa makosa ya usalama barabarani. Mtuhumiwa huyu alikamatwa tarehe 02/08/2014 huko Kata ya
Chamazi, Mbagala Majimatitu Mkoa wa Kipolisi Temeke akiwa amevalia sare za Polisi na cheo cha Stesheni Sajenti.

Baada ya kukamatwa alikutwa na gari namba T723 BAK T/Cresta rangi nyeupe analilotumia kuzunguka maeneo mbalimbali ya jiji kutapeli watu akiwadanganya yeye ni askari polisi. Gari hilo lilipopekuliwa lilikutwa na
  • Radio Call 1yenye namba GP380 aina ya Motorola
  • Leseni za udereva zipatazo 40 za watu mbalimbali
  • Stakabadhi 02 za Serikali zenye nambari A0531562 na A1672464
  • Police Loss Report mbalimbali.
  • Nakala 03 za Notification zilizojazwa.
  • Kofia moja ya (Uhuru Cape) ya Usalama barabarani,
  • Beji 01 yenye jina la E.R. MWAKYUSA ya kuweka kifuani.
  • Ratiba ya mabasi yaendayo Mikoani ya SUMATRA

S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
Mtuhumiwa