Taarifa ya mabadiliko ya muda wa saa za kazi katika ofisi za NHIF

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)

TAARIFA KWA UMMA


MABADILIKO YA MUDA WA SAA ZA KAZI KATIKA OFISI ZA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA


Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unapenda kuwatangazia wadau wake na wananchi wote kwa ujumla kuwa umebadili muda wa saa za kazi kwa ofisi zake kote nchini. Mabadiliko haya yanatokana na ukweli kwamba wadau wa Mfuko wanawahi sana kufika ofisi za Mfuko kupata huduma. (Uzoefu wa Mfuko unaonyesha wadau hufika kabla ya saa 2 asubuhi kupata huduma).

Hivyo, kuanzia tarehe 1 Agosti 2014 ofisi za NHIF zitakuwa wazi kuanzia saa moja na nusu (1.30) asubuhi hadi saa kumi kamili (10:00) jioni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

Huduma zote zinazotolewa na Mfuko zitaendela kutolewa kama kawaida muda huo na wote mnakaribishwa kuendelea kupata huduma za Mfuko kama kawaida.

NHIF: "Huduma bora za matiabau ni haki yako na ni dhamana yetu"

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Kaimu Mkurugenzi Mkuu,

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,

S.L.P.11360, Dar es Salaam; Simu: 022 2133969/964;

Barua pepe: [email protected]; Tovuti: www.nhif.or.tz